Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4. Mayai yana kiinilishe mhimu sana kiitwacho ‘Choline’Choline ndicho kiinilishe mhimu kabisa ambacho watu wanakikosa na watu wengine hawana habari kabisa juu ya uwepo wake.Ndiyo, ni kiinilishe mhimu zaidi na mara nyingi hupangwa pamoja na vitamini za kundi B.
 
Hiki ni kiinilishe kinachopatikana katika mayai ambacho kazi yake kuu mwilini ni kutengeneza ukuta wa seli na kinacho kazi pia ya kutengeneza molekuli za hisia katika ubongo na kazi zingine nyingi.Tafiti zinaonyesha zaidi ya asilimia 90 ya watu wanapata kiasi kidogo cha choline kati ya kile ambacho kimependekezwa kila mmoja ale kwa siku.Yai zima, lote, ni chanzo kizuri cha choline. Yai moja huwa na zaidi ya mg 100 za kiinilishe hiki mhimu ambacho watu wengi hawakijuwi.
 
5. Mayai hubadili msongamano wa chini wa lipoprotini kolestoMsongamano wa chini wa lipoprotini kolesto au kwa kiingereza ‘Low Density Lipoprotine’ (LDL) ndio ambao hujulikana kama ni kolesto mbaya.Inajulikana wazi, kuwa na msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto huleta uwezekano wa hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo.
 
Lakini kile watu wengi hawakifahamu ni kuwa huu msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto umegawanyika tena katika matawi madogo ambayo yanafanya jumla ya chembe chembe za msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto.Kuna msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto mdogo, kuna msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto wa kati na kuna msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto mkubwa zaidi katika hizo chembe chembe zinazounda msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto.
 
Hata kama mayai huwa na uwezo kidogo wa kuongeza kiasi cha msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto katika baadhi ya watu, tafiti zinaonyesha kwamba chembe chembe hizo hubadilika toka katika usawa mdogo hadi katika usawa wa kati hadi kuja kuwa katika usawa mkubwa ambao ni jambo zuri.
 
Moja ya viinilishe viwili mhimu zaidi katika kufanya kazi hiyo ni hivi vijulikanavyo kama Lutein na Zeaxanthin vipatikanavyo katika mayai, ambavyo ni viuaji sumu vyenye nguvu au vyenye kazi ya kuondoa sumu ambavyo hujijenga katika retina ya jicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…