Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti kama karoti. wataalamu wanashauri ili uwe na afya bora unatakiwa ule karoti sita kwa wiki au moja kwa siku. Unaweza kula karoti ya kuchemshaa,juisi au mbichi
 
Huifanya ngozi iwe nzui na yenye afya, kama utatumia kurutubisha ngozi yako, ikwangue kwa kutumia grater kiasi unachotaka tia asali mbichi kijiko 1 kikubwa (cha kulia chakula) mafuta ya nzai au olive kijiko kimoja kikubwa na limao kijiko 1 kikubwa changanya vizuri, kisha itumie kusugua mwilini sehemu yoyote unayotaka, ukimaliza acha kama dakika 15 na zaidi kisha oga, itasaidia kuondoa taka katika vinyweleo, kuifanya ngozi iwe laini na kuondoa mikunjo katika ngozi, Kumbuka inatakiwa asali mbichi na siyo asali yoyote.
 
Karoti hupunguza hatari ya kupata Shinikizo la Damu (blood pressure) kwani ulaji wa karoti husaidia mwili kupata madini muhimu ya Potassium ambayo husaidia kutanua mirija ya damu (bllod vessels na kufanya damu kufika katika maeneo husika ya mwili (organs).
 
Karoti husaidia kuongeza kinga mwilini (immune booster). Kwasababu tabaia asilia ya karoti kuwa na antibacteia pamoja na antiseptic ambazo husaidia kuzuia kinga za mwili. Pia Karoti ina Vitamin C muhimu kwa kusisimua seli nyeupe za damu (white blood cells) ambazo ni sehemu muhimu katika kinga ya mwili.
 
Mchanganyiko huo pia hutumika kama kinga dhidi ya saratani, matumizi ya juisi ya karoti yenye mchanganyiko wa tangawizi husaidia kuukinga mwili dhidi ya matatizo ya saratani za aina mbalimbali kwani husaidia kuua seli zinazoweza kuchangia matatizo ya saratani.
 
Hulinda meno na fizi, karoti pekee yake kwanza inatosha kwa kuwa mlinzi mzuri wa kinywa, hivyo matumizi ya glasi moja ya juisi ya karoti iliyochanganywa na tangawizi baada ya kula husaidia pia kulinda afya ya kinywa kwa ujumla.
 
Matunda hayo kwa pamoja yatahitajika kuandaliwa vizuri kwa kuyaosha na kutoa maganda pamoja na mbegu na kisha kuchanganywa kwa pamoja na baadaye kusagwa, huku ukianza na tufaa na matikitimaji na baadaye kuchanganywa kwa pamoja na karoti iliyosagwa .
 
Baada ya mchanganyiko huo kusagika unashauriwa kuchuja mara moja na kuweka kwenye jagi na baadaye kuongeza kiwango kidogo sana cha sukari au kutoweka kabisa, kisha utatumia mchanganyiko huo kunywa asubuhi na jioni kila siku kikombe kimoja . Fanya zoezi hilo angalau kwa miezi miwili mfululizo na itakusaidia katika kukukinga dhidi ya magonjwa ya mara kwa mara
 
Back
Top Bottom