Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wabunge mia moja waliotemeshwa ubunge CCM.

>Suleiman Sadiqq- Mvomero- nje
>Dalai Kafumu- Igunga, nje
>Mussa Ntimizi- Igalula, nje
>Ezekiel Maige- Msalala,nje
>Alaan Kiula- Iramba Mashariki nje
>Justin Monko- Singida Kaskazini-nje.
>Janet Mbene, Ileje
>John Kaduttu- Ulyankulu
>Anne Tubaijuka Muleba kusini-nje
>Salum Hamis Meatu.
>Hamud Jumaa- Kibaha, nje
>Haroon Pirmohamed- Mbalali.nje
>Rafael Gashaza- Ngala nje
>Hassan Masala-Nachingwea.nje
>Jumanne Maghembe-Mwanga, nje
>Jitu Soni-Babati vijijini -nje
>James ole Milya-Simanjiro -nje
>Omar Badwel- Bahi, nje
>Emanuel Papian- Kiteto, nje
 
Waliopoteza nafasi ya ubunge.

> Augostine Masele Mbogwe -nje
>Issa Mangungu -Mbagala, nje
>Geoffrey Mgimwa -Kalenga, nje
>Venance Mwamoto -Kilolo, nje
>Mahmoud Mgimwa Mufindi kaskazini.
>Edwin Sanda -Kondoa mjini
>Charles Kitwanga -Misungwi
>Oscar Mukasa -Biharamilo magharibi
>Pundensiana Kikwembe -Kavuu, nje
>Richard Mbogo -Nsimbo, nje
>Christopher Chiza -Buyungu. Nje
>Norman Sigalla -Makete. Nje
>Kangi Lugola -Mwibara nje
 
Tumia Muda Wako
Muda ni kitu muhimu sana katika maisha ya mtu yeyote. Kuna msemo walisema wazungu. “Time is money” wakimaanisha muda ni pesa. Ukitumia mda wako vizuri unaweza fanikisha mambo mengi sana. Muda haupotezwi bali muda hutumiwa vibaya. Kwa maana hiyo basi, tumia muda wako kufanya yale ambayo yanakuingizia faida katika maisha yako. Hepuka mambo yasiyoingiza chochote kizuri katika maisha yako. Hepuka michezo isiyo na faida katika maisha yako. Badala yake fanya mambo yenye faida na kama hauna kazi ya kukulipa basi waza na tafakari yale yatakayokuingizia faida katika maisha yako. La msingi tambua kwamba kila dakika katika maisha yako ina maana kubwa sana na endapo utapitisha dakika moja tu katika maisha yako kwa kufanya kisicho na faida basi jipange kujuta sana baadae.
 
Tumia Mda wa Wenzako
Nahisi hapa unaweza kupata utata juu ya maana ya hii nukta. Lakini maana yake ni hii hapa; Muda ambao mwenzako anautumia kulala unaweza kuutumia kupata faida na atakapoamka akastaajabu na kushangaa. Mataifa yaliyoendelea yana mfumo tofauti kabisa wa kufanya kazi ukilinganisha na mataifa yanayotazamwa kama mataifa yanayojukongoja katika maendeleo. Mataifa haya hutumia mfumo wa kufanya kazi kwa masaa 24 ikiwa na maana kwamba, hakuna mipaka katika kutafuta au kufanya kazi. Unapotafuta usiweke mipaka. Wanapolala wavivu basi wenye nia huinuka na kwenda kutafuta.
 
Tumia Watu
Kila unachotaka katika maisha yako kiko katika mikono ya watu. Kama ni pesa basi ziko mikononi mwa watu. Kama ni kazi basi ziko mikononi mwa watu. Tumia watu upate vya watu. Si lazima kuongea na wale unaowafahamu tu bali kila unayepata nafasi ya kuongea nae. Unatakiwa kuwa na mtandao wa kutosha katika maisha yako ili kufanikiwa katika maisha yako. Waambie watu wewe ni nani na unaweza nini ikiwezekana tumia hata matendo kudhihirisha maneno yako. Hakikisha kila mtu mpya unaekutana nae unaachana nae ukiwa na mtandao nae tayari. Omba awasiliano na ikiwezikena omba kuonana nae tena.
 
Tumia Mazingira
Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyokuzunguka katika maisha yako. Kila kinachokuzunguka kina mchango mkubwa sana katika kile unachokitaka katika maisha yako. Katika maisha yangu nilishaona mtu akisomesha watoto wake kwa kuuza chupa za plastiki alizokuwa akiokota katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Tumia mazingira yako kupata kile unachokitaka katika maisha yako. Tambua mazingira kutambua ni nini ufanye ili kufanikiwa katika kile unachokitaka katika maisha yako. Angalia mazingira yako yanahitaji nini na je ukiyapa kile kinachokosekana utaweza fanikiwa? Je ulishaona watu wakiuza maua? Ulishawahi kuona watu wakiuza miti? Ulishawahi kuona watu wakiuza maji? Tafakari na chukua hatua. Acha kuhofia kile unachohisi kitakufikisha katika kilele cha mafanikio ya maisha yako.
 
Tumia Teknolojia
Ulimwngu wa sasa unaongozwa kwa teknolojia ambayo kwa kiasi kikubwa bado haijaeleweka kwa watumiaji wake. Walio wengi wanatumia teknolojia kufanya mambo ambayo ya msingi hasa katika maisha yao. Watu wengi hutumia mitandao hasa ya kijamii kuchati, kutafuta wapenzi; jambo ambalo kwa namna moja au nyingine si baya, kunesha picha zao ambazo wakati mwingine huwaingiza matatizoni na hata kuleta migogoro isiyoisha. Lakini, ulishawahi kujiuliza ni wangapi wametumia mitandao hii kutangaza biashara yao? Wangapi wametumia mitandao hii kujiajiri ikiwa hata ni kwa mda tu? Amka na badili matumizi yako ya mitandao na badilisha matumizi yako kuwa yenye faida zaidi na si kwa maana ya kujilikana tu bila faida yoyote katika maisha yako.
 
Back
Top Bottom