Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Tumia Nguvu
Kila mwadamu ameumbwa na nguvu ya kipekee katika maisha yake. Hakuna mtu asiye na nguvu katika maisha. Tatizo ni kwamba watu walio wengi hawapendi kutumia nguvu zao walizonazo. Hapa siongelei nguvu ya nje ambayo mwanadamu anaweza kuwa nayo au asiwe nayo. Naongelea nguvu ya ndani kabisa ambayo kwa macho sio rahisi kuiona. Kile unachokihisi ndani ya moyo wako ndicho ninachokiongelea. Kile kilicho ndani yako kinachokuambia unaweza ndicho ninachokiongelea. Kama unaweza kuwaza kuwa na gari basi mungu amekupa nguvu ya kupata gari. Kama unaweza kuwaza kuwa mtu maarufu basi mungu amekupa nguvu ya kukufikisha hapo unapopaona. Cha kufanya ni kuamka na kuweka nguvu iyo katika matendo na kufanya unachoweza kufanikisha kile ambacho unahisi unaweza kukipata.