Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1595824942493.jpg
 
KISA CHA MWANAMKE MFUGA NYOKA NA FUNZO LA MAISHA YETU

Kuna mwanamke mmoja alipenda sana nyoka kiasi ambacho alichukua maamuzi ya kuwafuga

Alichagua nyoka mwenye rangi nzuri sana na yakuvutia alianza kumtunza na kumtimizia mahitaji yake yote na kama hiyo haitoshi basi alikuwa analala naye usiku mzima

Baada ya masiku mingi nyoka akawa mkubwa lakini akaanza tabia iliyompa mfugaji wake wasiwasi

Ilikuwa hali chakula karibia wiki nzima, na usiku ukifika huwa Halali kama ilivyokuwa zamani

Yule mwanamke akaamua kumchukua Yule nyoka na kwenda nae kwa daktari... Hofu ya mwanamke yule ni huenda kuwa nyoka wake anaumwa hivyo amuwahishe hospital kwa Msaada zaidi wa kiafya

Alipofika kwa daktari akamuelezea hali halisi anayomuona nayo nyoka wake

Yule daktari akamuuliza kuwa kama " je usiku unalala na huyu nyoka "?
Yule mwanamke akamjibu ndio

Daktari akamuuliza tena je usiku huwa anakuangalia sana??

Yule mwanamke akajibu ndio

Daktari akamwambia huyo nyoka ni chatu na hapo alikuwa anajiandaa ili akumeze... Hiyo kugoma kula chakula ilikuwa analiandaa tumbo Lake na hivyo kukutazama anatafuta timing za kuweza kukumeza kwa urahisi

CHA KUJIFUNZA

Kuna watu ambao wapo karibu yako ukidhani ni watu wema kwako ila ndani ya mioyo yao huyajui

Sio vizuri kumuamini kila mtu
 
BATA MAJI : maana halisi ya MAPENZI YA DHATI

Mpaka sasa hivi dunia bado inajiuliza kati ya pesa na mapenzi ni kipi kinaisumbua dunia

Kwa umri nilionao babu yenu nimeshuhudia na kusikia vifo vingi vitokanavyo na mapenzi kuliko vifo vitokanavyo na kukosa pesa

Nadhani ndio maana Ali kiba aliyaimba akisema yana Run dunia,
 
Ni kweli mapenzi yanatesa na kuumiza hasa ukijua thamani ya kupenda na unayempenda akajua thamani ya kupendwa

ndege aina ya bata maji ndio ndege waaminifu na wenye mapenzi ya dhati huenda kuliko hata binadamu

Bata maji ambao katika maisha yao yote Huwa na mpenzi mmoja tu

Na ikitokea mmoja wao akafariki basi huyo mwengine hubaki mpweke daima na muda mwengine huenda akafariki kutokana na upweke juu ya mwenza wake

Najua kuna watu wanatamani wapenzi wao kuwa bata maji 🤣🤣🤣🤣
 
Kathe ndiye mwanamke wa kwanza wa Australia kuhukumiwa kifungo cha maisha jela bila msamaha katika historia. Alipatikana na hatia ya mauaji ya mume wake John Price mwaka 2000, anatumikia kifungo chake huko Silverwater, Australia.
 
Back
Top Bottom