halikadhalika kwa watoto sio jambo jema sana kupenda kuwapa vitu vya sukari kwa wingi kama pipi, peremende n.k. Kwani huenda vikasababisha madhara katika meno yake
Ulaji ulio salama ni kati ya kushiba na kuwa na njaa. Yaani mtu anatakiwa kiafya asishibe sana kiasi cha kushindwa kujimiliki kama kukimbia n.k hivyo ale kwa ukati na kati
Unywaji wa maji ni jambo la umuhimu sana kwa afya. Wataalamu wa afya wanasisitiza sana, kwani maji yanaweza kupunguza hatari za ugonjwa wa UTI,maumivu ya kichwa na kurekebisha migongeo ya chakula tumboni
Mtu anatakiwa atumie muda katika kutafuna chakula. Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa mmeng’enyo wa chakula huanza rasmi mdomoni ambapo vyakula vya wanga huanza kumeng’enywa. Hivyo kama mlaji hatatafuna vizuri huenda asipate virutubisho kwa usahihi.
Unaweza ukadhibiti maradhi mbalimbali na mengi kwa kupangilia kula tu. Kwa msaada wa kanuni za afya unaweza kupambana na matatizo mengi ya kiafya kwa kurekebisha ulaji na kula kama inavyotakiwa.. Kwa mfano
Sio vizuri kulala ukiwa una jiko la mkaa likiwa lina moto. Wataalamu wa elimu za viumbe wanaeleza kuwa moto wa mkaa unatumia gesi ya okijeni kuwaka na badala yake hutoa gesi ya kabon monoksaid
Gesi hii huweza kuungana na oksijeni kutengeneza kabondaioksaid. Hivyo hali hii itapelekea matumizi makubwa ya gesi yaoksijen ambayo mwanadamu atakuwa anatumia. Kama yupo chumbani anaweza kukosa hewa kabisa ikiwa chumba ni kidogo.