Si vyema kuvaa nguo nyingi na za kubana. Watu wengi leo wanasumbuliwa na fangasi sehemu za siri na hujikuna sana. Wadudu hawa wanapenda sana sehemu za majimaji hasa za siri.
Si jambo jema kuvaa nguo mbichi hasa zile za ndani. Jambo hili kiafya si jema kwani linaweza kuwafanya fangasi waliopo sehemu za siri kukuwa vizuri na kumfanya mtu ajikune kwa muwasho
Unapojisikia haja ndogo au kubwa ni vizuri kuwahi haraka kwenda kuitoa. Haja kubwa au ndogo inaweza kupelekea matatizo ya kiafya kama haitatolewa kwa muda unaotakikana
Haja kubwa ikichelewa kutolewa inakuwa ngumu kwani mwili utaendelea kufyonza majimaji yaliyopo kwenye haja kubwa. Haja hii ikiwa ngumu inaweza kusababisha mipasuko au michubuko kwenye njia na kusababisha damu.
Pindi ukipata majeraha si vyema kuvyonza damu kwa mdomo. Kwani damu ile siosalama. Ni damu ambayo imekusanya vitu vingi kama urea, seli, plasma, homone n.k.Hivyo si vyema kuila damu hii.
Ni rahisi kwa wanawake kupata UTI kuliko wanaume. Ni kwa sababu wanawake mirija yao ya haja ndogo ni midogo, halikadhalika sehemu zao za haja ndogo nakubwa zipo karibu hivyo ni rahisi kwa vijidudu vya UTI kuingia njia ya haja ndogokwa kutokea njia ya haja kubwa
supu ya samaki inashauriwa sana na wataalamu wa afya. Bila kusahau mafuta ya samaki ambayo yana uwezo wa kupambana na saratani na kufanya ukuaji wa mtoto uwe salama.
Hakuna vyakula vilivyohakikiwa na wataalamu wa afya kuwa vinaongeza seli za CD4. Ila unaweza kuongeza uwezo wa mwili wako kupambana na maradhi kwa kula chakula bora na mlo kamili
Kama unatumia vidonge vya vitamini si vyema kula maini kwa wingi maana maini yana vitamini vingi hivyo unaweza kupata maradhi yahusuyo kuzidi kwa vitamini