Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1599404053075.jpg
 
“Bora ukosee kutafuta Mke/Mume, sio ukosee kuchagua maana majuto yake miaka 5, mkiwa na Diwani wa CCM fedha zikija zikichezewa nitashughulika nae mkimleta mwingine sina uwezo wa kumshughulikia, wa CCM nitamnyoosha hata kumfukuza uanachama, wa chama kingine siwezi kumfukuza”-JPM akiwa Simiyu
 
Mtu anakuja anasema mbona hamjapandisha mishahara?, ukishampandisha Mtu daraja mshahara wake haubadiliki?, tumerekebisha PAE kutoka 11% hadi 9%, tumelipa malimbikizo ya Wafanyakazi zaidi ya Bil 500 hiyo sio fedha!?”- JPM akiwa Mara

“Mambo ya kuwadanganya Wafanyakazi unawaongezea mshahara halafu kesho yake nauli zinapanda, unga,mafuta na kila kitu kinapanda hivyo vimepitwa na wakati lakini nimewaahidi Wafanyakazi kwamba kabla sijamaliza muda wangu nitawapandishia mishahara msijali”-JPM
 
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ilala, Christopher Myava amemuonya Hashim Rungwe ambaye ni mgombea Urais kupitia CHAUMMA kuwa kugawa chakula ‘ubwabwa’ wakati wa kampeni ni rushwa na ni kosa kisheria> “Watu wamwage sera sio kushawishi kwa rushwa”

Myava amesema Sheria inayohusu gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 inapiga marufu Mgombea kutoa vitu kama chakula kushawishi wapigakura ili wamchague, Rungwe amekuwa akiwaalika wafuasi wajae kwenye kampeni zake ikiwemo uzinduzi utakaofanyika Manzese, DSM leo Septemba 5 kwa kuahidi ubwabwa utakuwepo.

Rungwe amesema atatumia ubwabwa kama Vyama vingine wanavyotumia Wasanii, amesema kufanya hivyo si rushwa na amewataka wajiandae kupelekana Mahakamani.
 
“Baba wa Taifa Mwl.Nyerere mlimpa miaka 27, akaja Mwinyi mkampa miaka 10, akaja Mzee Mkapa (Mungu amlaze mahali pema) mkampa miaka 10, amekuja Kikwete mkampa miaka 10, Mimi nina dhambi gani mnataka mnipe miaka 5 tu!?, nawaomba nipeni miaka mingine 5 zaidi”-JPM akiwa Maswa
 
"Watoto wenu wana njaa, wanakwenda shule hawaelewi kitu sababu ya njaa, nitahakikisha wanapata ubwabwa, mimi nimewahi kulazwa Hospitali moja hapa DSM ila nikaondoka kisa njaa, hamna chakula Hospitali, kote nitapeleka ubwabwa” -Hasheem Rungwe akizindua kampeni za CHAUMMA Kitaifa katika eneo la Manzese DSM

“Hawa Polisi mnawaona hapa hawajalipwa mishahara, hivi mishahara si haki ya Mtu hiyo!?, Watumishi wote wa Serikali hakuna aliyeongezwa mishahara miaka mitano, hivi hii inawezekana kweli!?, hivi wao wanaopita huko na magari yao si wameshiba!?, tutaongeza mishahara”- Hasheem Rungwe
 
Back
Top Bottom