Newcastle imeweka dau la pauni milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji Callum Wilson na wanataka kukamilisha mchakato kwa ajili ya kumnyakua mchezaji huyo, 28 anayekipiga katika klabu ya Bournemouth kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi ya primia mwishoni mwa juma lijalo dhidi ya West Ham (Sunderland Echo)
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anataka kurejea Juventus, ambayo ndio sababu hajatia saini mkataba mwingine Old Trafford huku mkataba wake wa sasa unakamilika mwaka 2021. (Tuttosport)
Wachezaji wa Barcelona Luis Suarez,33 na Arturo Vidal,33, wamefanya mazoezi kando na wenzao siku ya Jumamosi wakati wote wawili wakijiandaa kuondoka kwenye klabu hiyo kuelekea Juventus na Inter Milan. (ESPN)
Crystal Palace inamuweka mshambuliaji wa Sassuolo Jeremie Boga kuwa mbadala wa Wilfried Zaha ingawa Napoli, Rennes, Atalanta na Bayer Leverkusen pia zinamuhitaji mchezaji huyo, 23. (Sky Sports)
Athari ya mshikano huo ilisafiri kwa takriban miaka bilioni ili kufika ardhini na bado zilikuwa na nguvu kuyumbisha vifaa vya kutambua mwanga nchini Marekani na Itali mnamo mwezi Mei mwaka uliopita.
Uchambuzi huo ndio wa hivi karibuni kutoka kwa kituo cha kimataifa cha LIGO-VIRGO, ambacho kinasimamia mifumo mitatu ya kutambua mawimbi ya mvuto nchini Marekani na Ulaya.
Inashangaza, kweli," alisema prof Nelson Christensen kutoka Côte d'Azur Observatory huko Ufaransa. "athari za Wimbi hilo zilisambaa kwa miaka bilioni saba.
Algorithms au mahesabu ya kompyuta zilibaini chanzo kuwa wakati wa mwisho wa mgongano wa mashimo mawili meusi yanayozunguka - moja lenye uzani wenye ukubwa mara 66 kuliko ule wa Jua letu, na jingine lenye uzani mkubwa mara 85 zaidi ya jua.
Kuhusika kwa kitu chenye uzito mara 85 ya jua letu kwenye mgongano kumewafanya wanasayansi wa kushirikiana kukaa chini kwa sababu uelewa wao wa jinsi mashimo meusi hutengenezwa kufuatia mlipuko wa nyota hawawezi kuwajibikia kitu kwa kiwango hiki.