Taarifa ya mtandao wa Daily Mail wa Uingereza Iliyochapishwa Aug 6, 2014 ilisema kuwa Adriana mwanamke wa umri wa miaka 39 na mumewe Leandro wa umri wa miaka 37 raia wa Sao Paulo Brazil walioana tangu mwaka 2004 na kupata watoto watatu.
Wiki chache baada ya Adriana kuzaliwa miaka hiyo 39 nyuma alitelekezwa na mama yake hali iliyofanya alelewe na watu baki kwa miaka yote na baadaye kumpata mume huyo, lakini muda wote huo alikuwa anaendeleza juhudi zake kumtafuta mama yake.
Mwaka 2014 Adriana alifanikiwa kumpata mama yake kupitia mahojiano fulani aliyokuwa akiyatazama katika TV, alivyomtafuta na kumfika mama akastaajabu kuona bintiye huyo ameolewa na kaka yake wa tumbo moja.