Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwaka 1994, Bill Gates akionesha diski ya CD-ROM huku akiwa amekaa juu ya furushi la makaratasi yaliyopangwa zaidi ya 330,000. Tafsiri ilikua ni kuonesha kwamba, Diski hiyo ina uwezo wa kuhifadhi vitu vingi na faida juu ya kulinda mazingira ambapo vitu hivyo pengine ilibidi vihifadhiwe kwenye makaratasi kama hivyo.
 
Wakati yuko shule Rebecca Townsend binti mdogo raia wa Conneticut US alijipa matamanio matatu aliyotaraji kuyafanya katika maisha yake kabla hajafa, moja ilikuwa ni kukiss kwenye mvua, pili ni kusafiri kwenda Spain na tatu ni kuokoa maisha ya mtu.
 
Kiss in the rainFly to SpainSave a lifeMiaka kadhaa baadaye, mwaka 2015 ni kweli alisafiri kwenda Hispania yeye na familia yake kwa matembezi akiwa na umri wa miaka 17, kabla ya kuondoka US alimkiss boyfriend wake wakiwa kwenye mvua.
 
Walisafiri hadi Hispania na kurudi, July 2, 2015 wakiwa Notre Dame, Indiana US mmoja wa wanafamilia wake Ben Arne alitakiwa kugongwa na gari barabarani, lakini kwakua Rebecca alimuwahi na kumsukuma asigongwe, Ben akapona na kugongwa yeye.
 
Hapo awali familia hii ya watoto wanne ililazwa hospitalini kwa siku kadhaa kwa maumivu makali ya tumbo baada ya kula chakula chenye sumu. Waliporuhusiwa waliandaa chakula cha jioni na majirani zao kufurahia afya baada ya kupona lakini waliishia kupata kisanga kingine.
 
Katika mji mdogo wa Hexham Uingereza Mei 5, 1957 wasichana wawili Joanna Pollock wa miaka 11 na mdogo wake Jacqueline wa miaka 6 waligongwa na gari na kufariki wakati wakienda kanisani na rafiki yao Anthony, hii iliwaumiza sana wazazi wao John na Florence.
 
Back
Top Bottom