Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Edinson Cavani
Mabao 50, mechi 116
Cavani amecheza soka la barani Ulaya kwa miaka 12, tangu alipojiunga na Palermo mwaka 2007. Na akaanza kuichezea timu ya Taifa ya Uruguay mwaka 2008, kwa sasa ndio mfungaji bora namba mbili wa muda wote ndani ya taifa hilo, pia ni ndio mfungaji bora namba moja ndani ya PSG, akiwa na mabao 200. Kwenye upande wa timu ya Taifa ana mabao 50 katika mechi 116.
 
Alexis Sanchez
Mabao 43, mechi 132
Watu wengi walimtabiria makubwa wakati anasajiliwa kwenda United akitazamiwa kuwa anakwenda kusaidia kuinyanyua timu hiyo kutoka pale ilipokuwa kwenda sehemu nyengine, lakini hilo lilishindikana na alifeli, lakini wakati anafeli kwenye upande wa timu ya taifa bado anaendelea kukamua ile mbaya na yeye ndio mfungaji bora wa muda wote na akiwa na mabao 43, katika mechi 132. akiisaidia timu hiyo kushinda mataji mawili mfululizo ya Copa America, mwaka 2015 na 2016.
 
Mohamed Salah
Mabao 43, mechi 68
Akiwa amecheza michezo 68, na kufunga mabao 43 tayari anatishia kuwa huenda akavunja rekodi ya mkongwe Hossam Hassan ambaye ndio mfungaji bora wa muda wote wa Misri akiwa na mabao 67, baada ya kucheza mechi 176. Katika ngazi ya klabu ameshashinda mataji yote, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu ya England baada ya klabu hiyo kulikosa kwa miaka 30
 
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…