YUKO ANAYEKUPENDA ZAIDI*
BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu."
Yeremia 31:3
Kama Kuna Jambo la Muhimu katika Maisha ya Mwanadamu, mojawapo ni KUPENDWA, Kwa Bahati mbaya Sana tunaishi katika Kizazi kinachozidi kupoteza Ladha ya Upendo Katika Jamii kila kunapokucha. Katika Jamii, katika Ndoa, katika Mahusiano, Makazini, vyuoni na Mashuleni, Sehemu za Kutolea huduma, Kati ya ndugu n.k. Upendo unazidi kutoweka.
Unaweza kuwa mmoja wa wahanga wa Kukosa KUPENDWA, unaweza kuwa unapitia Kusalitiwa au kuchukiwa bila Sababu, na hatimaye kukosa Amani, JIPE MOYO, Bado lipo tumaini, hebu isikie Sauti ya Mungu inayosema "Naam Nimekupenda kwa Upendo wa Milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu".
Ni fahari Kubwa kuutumaini Upendo wa Mungu kuliko Upendo wa Wanadamu usiodumu.
Asante Baba Mwema, tunashukuru kwa Upendo wako mkuu, endelea kutuliza mioyo iliyojeruhiwa kwa kukosa Upendo.
NAWATAKIA JIONI NJEMA.