Mieleka ni mchezo wa maigizo lakini yenye uhalisia, Kila kinachofanyika kimepangwa tayari na wapiganaji huwa wanajua lakini unachokiona kina uhalisia ndiyo maana kuna muda watu huumia. Kwa ufupi Mieleka' wanakuonesha kile wanachotaka uone na sio uhalisia wa kinachotokea.
Jamii ya Tidong, Indonesia hutaruhusiwa kuuona uso wa bi harusi wako hadi umuimbie nyimbo kadhaa za mapenzi zitakazompendeza wakati wa kufunga ndoa. Pia baada ya ndoa waliooana hawaruhusiwi kuingia bafuni na chooni kwa muda wa siku 03 kuepusha mikosi katika maisha yao.
Korosho husaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, huongeza kinga ya mwili, huongeza uwezo wa kuona, husaidia kupunguza uzito na zaidi husaidia kuongeza nguvu za kiume.
Sokwe' wana uwezo wa kujifikiria kuhusu uwezo wao wenyewe, Mfano Wana uwezo wa kubuni njia mbalimbali za kutatua matatizo, uwezo ubora na mapungufu yake binafsi n.k