Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Miongoni mwa viumbe hatari zaidi vinavyopatikana kwenye maji ni aina ya samaki anayefahamika kwa jina la (Eel),

uhatari mkubwa wa samaki huyu ni kwamba mwili wake una uwezo wa kuzalisha umeme wa mpaka kufikia volti 650.

Samaki huyu ana uwezo wa kuyapa maji shoti ya volti zaidi ya 600 ili tu kufanikiwa kumdhuru kiumbe yeyote ndani ya maji. Kiumbo anaweza kukua kwa urefu mpaka futi 8 au mita 2.5 na awapo kwenye maji hufanana na nyoka.

Zipo baadhi ya video zinazoonyesha baadhi ya watu tofauti tofauti ulimwenguni wakionekana kupoteza maisha ghafla kwa mtetemesho wawapo ndani ya maji na wengi wao wamethibitishwa kufariki kutokana na shoti ya samaki huyo.
 
Ubre alizaliwa mwaka 1972, alikuwa ng'ombe maarufu sana na ng'ombe pendwa kwa aliyewahi kuwa kiongozi na mwanamapinduzi wa taifa hilo Fedel Castro, umaarufu wake mwingine ulitokana na kasi yake ya kuzalisha maziwa.

Katikati ya mwaka 1982 Ubre alikuwa ana uwezo wa kutoa mpaka lita 110 za maziwa kwa siku moja, kiwango cha juu zaidi kwa ng'ombe mmoja kukitoa.Kutokana na hilo Castro alitokea kumpenda sana ng'ombe huyu hadi kufikia hatua kumtaja mara kwa mara hata katika hotuba zake.Ubre alifariki mwaka 1985 huko Nueva Gerona ambapo licha ya kupewa heshima ya kijeshi na mapumziko ya kitaifa lakini pia amejengewa sanamu yake mjini Nueva Gerona Cuba kama njia ya kumkumbuka.
 
Nchini Bangladesh katika mji mdogo wa Rajshahi kuna familia moja ya bwana aitwaye Amal Sarker na mwanawe aitwaye Apu Sarker na watoto wa kiume wa familia hiyo wamekuwa na kilema kinachojulikana kama "Adermatoglyphia" ambapo familia hiyo haina alama za mikononi au vidoleni "Fingerprint" na pia husababisha ngozi zao kuwa kavu na viganja vyao vya mikono na miguu huwa na joto kali.
 
Nchini Bangladesh katika mji mdogo wa Rajshahi kuna familia moja ya bwana aitwaye Amal Sarker na mwanawe aitwaye Apu Sarker na watoto wa kiume wa familia hiyo wamekuwa na kilema kinachojulikana kama "Adermatoglyphia" ambapo familia hiyo haina alama za mikononi au vidoleni "Fingerprint" na pia husababisha ngozi zao kuwa kavu na viganja vyao vya mikono na miguu huwa na joto kali.
 
Cassowary anaitwa ,Ni jamii ya Ndege wanaopatikana Australia, ni ndege hatari zaidi Duniani ,muone hapo kama mzembe mzembe tu,Sifa za huyu ndege yeye akihisi hatari yaani akikuhisi unataka kumuua, anaruka juu anakuvamia na shambulio lake ni kama umepigwa na silaha hizi za kisasa kama AK47 na majeraha yake lazima ufe , yeye anapokuvamia huvaa mask anayo yake ya asili , Kifupi huyu ndege huitwa Muuaji wa watu.Mbaya kuliko zote huyu nyama yake utachemsha mawe yakaiva nyama ya huyu bado haijaiva..
 
Jumba la Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson ambalo alilinunua mwaka 1987 kwa USD milioni 19.5 limenunuliwa na Tajiri Ron Burkle kwa kiwango kinachotajwa kufika USD milioni 22 (USD milioni moja ni sawa na Tsh. Bilioni 2.3 )Jumba hilo ambalo lipo Los Olivos, California likijulikana kwa jina maarufu la ‘Neverland’ likiwa ndani ya hekari 2700 na humo ndani lina zoo ya Wanyama mbalimbali kama Tembo na Twiga.Ron Burkle ni miongoni mwa Wamiliki wa Team ya mchezo wa Magongo unaochezwa kwenye barafu ya Pittsburgh Penguins,

Michael Jackson alifariki mwaka 2009 kwenye jumba jingine alilokua anaishi Los Angeles Marekani.
 
Inaelezwa kuwa injinia Nigel alikua anapenda sana bata hadi kufikia treni mpya ya LNER Class A4 4468 Mallard iliyoanza safari zake nchini humo mwaka 1938 kupewa jina hilo la bata, treni hii ilianza safari katika reli aliyoisimamia yeye wakati wa ujenzi kama injinia.

Treni inaitwa LNER Class A4 4468 Mallard, sasa hiyo Mallard mwishoni maana yake bata, ni ndege wanaofanana kwa asilimia 100 na bata, kuna duck na mallad, wote ni bata, kwahiyo waliipa treni jina hilo la bata kwa heshima ya jamaa kupenda sana ndege hao.

Sasa mwaka 2016 ikiwa inatimia miaka 75 tangu mtaalamu afariki mwaka 1941, serikali ikazindua sanamu yake hiyo iliyopo katika stesheni ya treni ya King's Cross huko London kama heshima ya kumkumbuka kwa utaalamu wake mkubwa katika usafiri wa treni nchini humo.

Sanamu ilimuonyesha yeye akiwa amesimama huku mguuni kukiwa na sanamu ya bata aliyeonekana amesimama naye kufuatia injinia huyo kua na mapenzi makubwa sana kwa bata enzi za uhai wake, kwani hata moja ya treni ilipewa jina la bata kwaajili yake.

Familia ya injinia ilikitafsiri kitendo hicho kama ni dhihaka kwa ndugu yao, walikasirika, hivyo siku chache tuu mbeleni watu walishangaa kuona sanamu ya bata pale mguuni imeng'olewa
 
July 8, 2020 mtandao wa the Sun wa Uingereza uliandika taarifa ya mwanaume Khalaf Ismail raia wa Minya Misri kumfungia dada yake Fadia wa umri wa miaka 50 katika chumba kwa miaka 22 tangu akiwa na miaka 28 kisa alikua anauliza sana kuhusu haki yake ya kupata urithi wa mali.

Inaelezwa kuwa baada ya kaka yake huyo kukereka na maswali hayo ya dada yake aliamua kwenda kumfungia katika chumba kimoja kwenye nyumba chafu huku akipelekewa chakula kidogo kila siku,

Fadia hakuwahi kutoka chumbani humo kwa miaka 22.

Majirani ndio waliogundua uwepo wa mtu ndani na kuanza kupata mashaka, na hata baada ya kumuona Fadia ambaye hali yake ya kiafya ilionekana kuwa mbaya, alikataa kabisa kurudi kuishi na kaka yake.

Kaka yake alikamatwa huku serikali ikiandaa kumpa pensheni Fadia ili aishi mwenyewe bila utegemezi wa kaka yake huyo.
 
November 13, 2000 mfanyabiashara Dariusz Janiszewski raia wa Wrocław nchini humo aliondoka ofisini kwake akidai kuwa anakwenda kuonana na mteja wake mahala, na hakurejea tena.

Inaelezwa kuwa mteja huyo alimtaka wakutane mahala waongee wawili tuu.Mwezi mmoja baadae December 10, 2000 mvuvi mmoja aliuona mwili wa Dariusz kando ya mto Odra ukiwa na kitanzi shingoni na mikono imefungwa na kamba kwa nyuma Uchunguzi wa maiti ulibaini kuwa inawezekana marehemu aliteswa na kutupwa mtoni kabla ya kufariki, lakini hadi kufika katikati ya mwaka 2001 polisi hawakumpata mhusika wa mauwaji hayo na kuamua kuufunga uchunguzi, hawakuendelea tena kuichunguza kesi hiyo.

Mwanzoni mwa mwaka 2003 polisi mpelelezi Jacek Wróblewski akaanza kuichunguza tena kesi hiyo baada ya kugundua kuwa simu ya marehemu haikuonekana baada ya kupotea, kwakua IMEI ya simu ilikuwepo wakaanza kuifuatilia kwa mtandao, ilikuwa inatumika bado japo ilikuwa imeuzwa mara kadhaa.

Waligundua kuwa kwa mara ya kwanza simu ya marehemu iliuzwa November 17, 2000 ikiwa ni siku nne baada ya marehemu kupotea, muuzaji alijiita Chris B.7 ambaye baadaye ilijulikana jina lake halisi ni Krystian Bala mwandishi wa riwaya nchini humo.

Walipomchunguza Bala waligundua kua miezi michache nyuma aliandika riwaya ya Amok inayoelezea mauwaji hayo hayo ambayo polisi wamekua wakiyachunguza kwa muda mrefu, pia waligungua kua Bala amekua akiandika maandiko mengine kuhusu unyanyasaji kingono ambao ni kweli umekua ukiripotiwa kufanyika.

Kesi hii iliendelea kuchunguzwa zaidi mpaka mwaka 2007 huku mtuhumiwa mkuu akiwa ni Bala ambapo baadaye alikutwa na hatia ya mauwaji na unyanyasaji kingono na kufungwa jela miaka 25.
 
Ilikuwa ni miezi 7 baada ya kuzikwa, papa aliyeingia madarakni baada yake Stephen VI aliamuru mwili ufukuliwe na uletwe mbele ya mahakama kusomewa mashitaka. Alimshtumu Formosus kwa uwongo na kwamba alikuwa amekubali upapa kinyume cha sheria.

Kesi ikafungwa kwa kuonekana Upapa wa Farmosus ulikuwa batili, akazikwa tena eneo tofauti na lile alilozikwa mwanzo kutokana na kutokuwa na sifa za kuzikwa hapo.

Baada ya miaka 13 kesi ikafufuka upya tena, madai ni yale yale kwamba jamaa alikubali kuwa papa kinyume cha sheria, ikaamriwa mabaki yake sasa yachomolewe kichwa, yaani iwe kama amekatwa kichwa kwa makosa hayo, akazikwa upya.

Miaka 10 baadaye tena kesi ikaamka upya, madai yakikwa ni yale yale kwamba Farmosus alijivika Upapa bila kufuata sheria, maamuzi ya mahakama sasa yakawa mwili wake ufukuliwe na utupwe mtoni, kwamba hakufaa kuzikwa, ikawa hivyo.
 
Marie alizaliwa Ufaransa July 2, 1882 na kufariki September 21, 1962. Huyu ni ndugu wa karibu, mjukuu wa Napoleon mtawala wa Ufaransa, alikuwa ni mtafiti wa maswala ya ngono, alikuwa anapenda kuandika kila alichokijua kuhusu ngono kutoka kwake binafsi ama kutoka kwa wengine pia.

Alikua anaandika wazi kuhusu maisha yake ya ngono na namna anaweza kuridhika, ndipo watu wengi walipojua kuhusu maisha yake na mumewe Prince George waliodumu kwenye ndoa yenye furaha kwa miaka 50 lakini hawakua wakifanya ngono kwakua mumewe alikua anavutiwa na wanaume wenzie.

Marie alijiingiza katika harakati hizi za kingono mwaka 1924, alikuwa anafanya uchunguzi wa maswala ya ngono kwa masaa mawili kila siku akishirikiana na mtaalamu Freud raia wa Australia.

Mwaka 1925 Marie alibaini kuwa umbali wa kisimi na uke unasababisha mwanamke asipate raha na msisimko wa ngono, akaamua kuwapima wanawake 243 urefu wa mtaro wa sehemu zao za siri na kugundua kua kisimi cha mwanamke kipo umbali wa centimeters 2.5 kutoka kwenye uke hivyo kumnyima msisimko mwanamke wakati wa ngono.

Aliamini kuwa wanawake wenye urefu huo hawawezi kukifikia kilele cha msisimko wa ngono kirahisi kulinganisha na wanawake wenye visimi vilivyo karibu zaidi na uke.

Kwa bahati mbaya Marie alichukua utafiti wake mbali sana, yeye na mtaalamu wa magonjwa ya wanawake wa Austria Josef Halban walianzisha upasuaji ambapo walikuwa wanakata mishipa ya kisimi na kukisogeza karibu na uke, wa kwanza kufanyika upasuaji huo alikuwa ni Marie mwenyewe mwaka 1927.

Lakini licha ya upasuaji huo, alisema bado hahisi raha ile aliyoitarajia wakati wa ngono na mpaka anafariki mwaka 1962 alikuwa aaaendelea kuandika mengi kuhusu ngono hasa kwa wanawake na kubaki kuwashangaza wengi.
 
Marie alizaliwa Ufaransa July 2, 1882 na kufariki September 21, 1962. Huyu ni ndugu wa karibu, mjukuu wa Napoleon mtawala wa Ufaransa, alikuwa ni mtafiti wa maswala ya ngono, alikuwa anapenda kuandika kila alichokijua kuhusu ngono kutoka kwake binafsi ama kutoka kwa wengine pia.

Alikua anaandika wazi kuhusu maisha yake ya ngono na namna anaweza kuridhika, ndipo watu wengi walipojua kuhusu maisha yake na mumewe Prince George waliodumu kwenye ndoa yenye furaha kwa miaka 50 lakini hawakua wakifanya ngono kwakua mumewe alikua anavutiwa na wanaume wenzie.

Marie alijiingiza katika harakati hizi za kingono mwaka 1924, alikuwa anafanya uchunguzi wa maswala ya ngono kwa masaa mawili kila siku akishirikiana na mtaalamu Freud raia wa Australia.

Mwaka 1925 Marie alibaini kuwa umbali wa kisimi na uke unasababisha mwanamke asipate raha na msisimko wa ngono, akaamua kuwapima wanawake 243 urefu wa mtaro wa sehemu zao za siri na kugundua kua kisimi cha mwanamke kipo umbali wa centimeters 2.5 kutoka kwenye uke hivyo kumnyima msisimko mwanamke wakati wa ngono.

Aliamini kuwa wanawake wenye urefu huo hawawezi kukifikia kilele cha msisimko wa ngono kirahisi kulinganisha na wanawake wenye visimi vilivyo karibu zaidi na uke.

Kwa bahati mbaya Marie alichukua utafiti wake mbali sana, yeye na mtaalamu wa magonjwa ya wanawake wa Austria Josef Halban walianzisha upasuaji ambapo walikuwa wanakata mishipa ya kisimi na kukisogeza karibu na uke, wa kwanza kufanyika upasuaji huo alikuwa ni Marie mwenyewe mwaka 1927.

Lakini licha ya upasuaji huo, alisema bado hahisi raha ile aliyoitarajia wakati wa ngono na mpaka anafariki mwaka 1962 alikuwa aaaendelea kuandika mengi kuhusu ngono hasa kwa wanawake na kubaki kuwashangaza wengi.
 
Mmoja ya wasaidizi hao 7 alikuwa ni St. Laurence ambaye kabla ya Kifo hicho kibaya cha kuchomwa na mafuta motoni aliomba apewe siku 3 ili apate muda wa kugawa mali zake zote kwa wagonjwa, vipofu na masikini wa mji huo ndipo auliwe.

Papa Sixtus II na Wasaidizi wake 7 akiwemo Laurence, waliamriwa kuuwawa na Mtawala Velerian mwaka 258 AD kwa makosa ya kuhubiri amani huku wakimtaja mtawala wao huyo kuwa ni mtawala asiyefuata misingi ya kiutawala, alikuwa na utawala kandamizi.

Katika kipindi cha utawala wake hasa mwaka 258, viongozi wengi wa dini kama maaskofu, mapadri, na mashemasi waliuawa kisa ni kumkosoa mtawala huyu kwa utawala wake kandamizi, hakutaka viongozi wa dini kuhubiri kuhusu utawala wake mbovu. Papa Sixtus II alikuwa mmoja wa waathirika wa kwanza wa mateso haya, alikatwa kichwa na kurostiwa kwenye mafuta Agosti 6, 258 AD.

Siku hiyo aliuawa pamoja na Wasaidizi wake wake 6 wa kanisa, Januarius, Vincentius, Magnus, Stephanus, Felicissimus na Agapitus. Msaidizi wake mmoja ambaye ni Laurence yeye aliomba auliwe siku 3 baadae ili apate muda wa Kugawa mali zake zote kwa masikini na wagonjwa, akapikwa na mafuta motoni Agosti 10, 258 AD siku nne baada ya Askofu wake.

Inaelezwa kuwa Laurence wakati anachomwa alikuwa akionysha Uso wenye tabasamu mpaka anakata Roho.

Hata hivyo mtawala 'Valerian' nae aliuwawa Mwaka 260AD akiwa mafichoni huko Iran baada ya kujulikana kuwa alikuwa anaiuza Roma kwa wapinzani katika vita mbalimbali hali iliyopeleka Roma kupigwa, kunyang'anywa mali, ardhi na raia wake kuteswa.
 
Kituo hicho maalumu kwa utafiti wa kansa na wagonjwa wa kansa kinaitwa Terry Fox Memorial Lookout kilichopo Ontario Canada, ukifika tuu unakutana na sanamu yake kubwa kama hio pichani.

Majina yake ni Terrance Stanley Fox, alizaliwa July 28, 1958 na kufariki June 28, 1981 (22) huko Canada kwa maradhi ya kansa, ilikuwa ni baada ya kutembea kwa miguu kwa siku 143 kuzunguka maeneo mbalimbali nchini humo kuomba michango kijengwe kituo maalumu kwa wagonjwa wa kansa.

Hata wakati anaanza safari hizo zilizofika kilomita 5373 alikuwa amekatwa mguu wake wa kulia kutokana na maradhi hayo. Mwaka 1982 serikali ya Canada ilijenga kituo kikubwa cha utafiti wa kansa na maalumu kwa wagonjwa wa kansa ili kumuenzi Terry.
 
Ilikuwa ni mwaka 1842 miaka minne baada ya mguu wake kukatwa, lilichimbwa kaburi na mguu huo ukazikwa kwa heshima zote za kijeshi ikijumuisha hotuba maalumu, sala, kanuni na mashairi yaliyosomwa kwa heshima mbele ya umma, kulikua na mapumziko ya kitaifa pia.

Mguu huo wa kushoto ulizikwa chini ya mnara katika maakaburi ya Santa Paula Mexico.

Anaitwa Antonio López de Santa Anna rais wa awamu ya 8 wa Mexico aliyeiongoza nchi hiyo katika vipindi tofauti tofauti, kipindi cha mwisho ikiwa ni mwaka 1853 hadi 1855. Yeye alifariki mwaka 1876 akiwa na umri wa miaka 82.

Mguu wake huo ulikatwa baada ya kuumizwa vibaya katika vita dhidi ya Ufaransa mwaka 1838, baada ya miaka minne mwaka 1842 akaamuru mguu huo uzikwe kwa heshima hizo zote.

Pichani ni mfanano wa mguu huo uliopo katika jumba la makumbusho ya kijeshi la Illinois State Military Museum huko Illinois US. Marekani wanamchukulia Santa Anna kama dikteta aliyewafukuza kinyama wamarekani nchini Mexico wakati akiwa madarakani
 
Hali hii ya ajabu ilianza kumtokea mwaka ya 1830 akiwa na miaka 32 akifundisha darasa moja lililokuwa na wanafunzi 17 huko Latvia, yeye hakuingia darasani, lakini alionekana pacha wake (mzimu) aliyeingia darasani hapo na kufanya kila kitu ambacho yeye hufanya.

Wanafunzi pia walikuwa wakiripoti kuwa Emilie anapokuwa ubaoni anaandika sentensi pacha wake huyo anajichomoa kutoka kwake na kuanza kuiga kile Emilie anafanya pale pale, wanafunzi walikuwa wakiona lakini yeye hakua akiona lolote.

Wakati mmoja Emilie alikuwa akimsaidia mwanafunzi kujiandaa kwenda katika sherehe maana ilikuwa shule ya bweni, ghafla mwanafunzi anaona anasaidiwa na akina Emilie wawili wanaofanana kila kitu, akazimia. Mambo haya yalipozidi akafutwa kazi.

Kutokana na kupenda sana kazi yake, Emilie alipata kazi katika shule nyingine ambayo alifukuzwa pia kutokana na mambo haya ya ajabu, yaani mtu mmoja anaonekana sehemu mbili katika muda huo huo, yeye hakua anajua chochote, alifukuzwa kazi katika shule 18 kwa mtindo huu.

Mwaka 1846 Emilie aliajiriwa tena kama mwalimu katika shule nyingine ya wasichana, hiyo ilikuwa kazi yake ya 19 na ya mwisho, baada ya hapo haijulikani ni nini kilichotokea kwa Emilie na pacha wake huyo waajabu.
 
Majina yake ni Aisin Gioro Puyi, alizaliwa february 7, 1906 na kufariki october 17, 1967 akiwa na miaka 61. Kwa mara ya kwanza alipewa utawala mwaka 1908 akiwa na umri wa miaka miwili na miezi 10 tuu akirithi kutoka kwa binamu yake.

Puyi aliishi kifahari, katika miaka yake ya mwisho madarakani alikuwa analindwa na walinzi 1000, madaktari 100 na alikuwa na wapishi 200. Alikuwa anaishi katika jumba ambalo hakuna yeyote anayeweza kufika.

Katika miaka yake yote madarakani alikuwa mtu wa kufanyiwa kila kitu, hata kuosha meno yake mwenyewe alikuwa anafanyiwa na walinzi aliowaajiri, hata kufunga kamba za viatu vyake mwenyewe haikua kazi yake.

Mwaka 1949 chama cha kikomunist kiliingia madarakani chini ya Mao Zedong na kutaka kumnyonga Puyi kutokana na utawala wake, lakini akaishia kufungwa jela miaka 10, alifariki mwaka mwaka 1967 kwa saratani ya figo.
 
Gladys aliyezaliwa mwaka 1896 huko Minneapolis US alikuwa mrukaji na maparachuti na mchezaji wa michezo hatarishi Kama hiyo aliyekuwa maarufu sana miaka hiyo huko US, umaarufu wake mkubwa ulitokana na michezo yake hii hatari ya kuruka.

Moja kati ya matukio yake hatari ilikuwa ni kutembea juu ya bawa la ndege akiwa amefunikwa macho mwanzoni mwa miaka ya 1920, huku ndege ikiwa angani.

Mwaka 1921 Roy alivunja rekodi ya kuruka na parachuti kwa mwanamke kwa umbali mrefu zaidi angani, aliruka kwa umbali wa futi 16,000, hii ilikuwa mara yake ya tatu kuruka katika umbali unaokaribiana na huu.

Kazi hizi zilikuwa zikimpa kipato cha pesa ya Tanzania 200,000 hadi 400,000 kwa wakati huo ambazo ni sawa na 5,000,000 hadi 10,000,000 za leo. Mwaka 1924 alitangazwa kama mwanamke nguli kwa urukaji kwa parachuti ulimwenguni, na alikuwa binti wa miaka 27 tuu.

Lakini pengine tukio lake la kukumbukwa zaidi ilikuwa ni tukio la mwaka 1925 alipocheza tennis juu ya bawa la ndege iliyokuwa hewani akiwa na Ivan Unger, haijulikani kama walikuwa wanacheza kweli au walijifanya wanacheza, lakini walionekana wakicheza juu ya bawa la ndege, ikiwa angani.

Matukio haya na mengine mengi ya hatari yalimfanya kuwa mwanamke maarufu sana duniani mpaka anapofariki Augost 15, 1927 (30) baada ya nguo yake kuvutwa na propeller la ndege iliyokua inajiandaa kuruka, alikuwa anataka kupigwa picha kabla ya kusafiri na ndege hio kwenda Roma.
 
Back
Top Bottom