Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Hii ndio rekodi ya dunia ya utunzaji wa kijusi kwa muda mrefu zaidi, miaka 27 mbele ya kijusi kingine kilichotunzwa kwa miaka 24, hiki mtoto alizaliwa November 25, 2017 huko Tennessee US, anaitwa Emma Gibson.
Vijusi vya Emma na Molly vyote vilianza kutunzwa siku moja ya November 14, 1992 ambapo kijusi kimoja kilipandikizwa kwa Tina Gibson mwaka 2017, na kingine kikaja kupandikizwa kwa Tina huyo huyo tena mwaka huu 2020, kwahio Emma na Molly ni mtu na dada yake.
Viini tete hivi hununuliwa na baadhi ya vituo vya kitaalamu kutoka kwa watu ambao husema hawana mpango wa kuzaa kutokana na umri kwenda au vinginevyo, hivyo badala ya kutoa mimba wanaenda kuuza vijusi hivyo vinavyohifadhiwa na kupandikizwa kwa wahitaji wa mtoto.
Mwaka 2016 Tina Gibson na mumewe Benjamin walifika katika kituo cha NEDC, National Embryo Donation Center Tennessee US kwaajili ya kuangalia uwezekano wa kupandikizwa kijusi, hatimae 2017 walifanikiwa na safari ya kukua kwa kijusi hicho kilichohifadhiwa tangu mwaka 1992 ikaanza, na 2020 wakafanikiwa tena.
Ukipandikizwa kijusi ujauzito unaanza kukua kuanzia muda ule ule kijusi kilivyotolewa na kuanza kutunzwa, kama ni wiki 8 au vinginevyo, miezi 9 baadae unajifungua kawaida kabisa. Kama una mume basi anakua hana ufanano wowote na mtoto huyo kutokana nayeye kutohusika kabisa katika uzalishaji.
Wakati akihojiwa na CNN Tina mwenye umri wa miaka 29 sasa alisema "ninachojali mimi nimepata mtoto baada ya kuhangaika miaka mingi, haijalishi imevunja rekodi ya dunia au lah. Ni zawadi yangu ya Christmas kutoka kwa Mungu."
Takwimu zinaonyesha kuwa karibia asilimia 5 ya watoto wote waliozaliwa US mwaka 2017 walitokana na usaidizi huu wa teknolojia