Ilikuwa ni mwaka 2007 ambapo msichana mmoja alikuwa akitembea katika pwani ya bahari katika kisiwa cha Jedediah Canada, akakutana na kiatu kimoja ambacho baada ya kukitazama akastaajabu kuona mguu upo ndani yake ukiwa na socks.
Tangu wakati huo miguu ya aina hio Ikiwa ndani ya viatu iliendelea kuokotwa katika pwani ya kisiwa hicho huku kusijulikane nini chanzo, kwasababu hakukuwahi kupatikana viungo vingine tofauti vya mwili zaidi ya vipande vya miguu vikiwa ndani ya viatu.
Miguu iliendelea kuokotwa zaidi hadi ilifika miguu mitano, hakuna aliyeweza kufahamu kwanini inaokotwa miguu hio, na hakukuwahi kutolewa taarifa zozote labda mtu kutekwa, kuvamiwa au kupotea, na hakukuwahi okotwa viungo tofauti na hivyo.
Mguu wa kwaza uliokotwa Augost 20, 2007, wapili Augost 26, 2008, watatu February 2, 2008, wanne Mei 22, 2008 na wa tano uliokotwa Juni 16, 2008.
Mmoja wa miguu iliyookotwa mwaka 2008 ulifananishwa na mguu wa mwanaume mmoja aliyejiua kwa kujirusha darajani siku chache nyuma lakini familia yake iligoma kutoa ushirikiano, na mwili wake haukupatikana, na miguu mingine waliamini ni ya watu hao pia waliokuwa wakijiuwa.
Lakini swali likaja, kuna uhusiano gani wa mtu kujiua kwa kujirusha darajani na kujikata au kukatwa mguu? Ukizingatia pia katika miezi hiyo iliokotwa miguu mitano, na watu waliojiuwa kwa njia hio walikuwa wawili pekee.
Wengine waliamini labda ni miguu iliyokuwa inatokana na ajali za ndege baharini hivyo ilikuwa ikisafiri kuja ufukweni huku wengine waliamini labda ni miguu ya wahanga wa Tsunami ya mwaka 2004 huko Asia hivyo miguu yao ilikuwa ikivutwa na maji baharini hadi kisiwani humo, lakini kwa miaka hiyo mitatu miguu si ingekua imeharibika vibaya?.
Waliamini zaidi baada ya kuona muundo wa viatu unafanana, na ni toleo lililotoka kabla ya mwaka 2004. Hizi ni imani tuu lakini ukweli hadi sasa hakuna uchunguzi ulioleta majibu sahihi juu ya swala hili.