ahsante sana, sikuwa nayafahamu hayo.
kwa tafsiri yako ni kwamba walimsaliti na kumkomoa mzee jumbe
Chanzo cha yote ilikuwa ni madai ya msingi ya
Wazanzibar.
Walikuwa na vikao Afisi kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar.
Walishambuliana hatimaye walikubaliana waende Dodoma wakiwa na madai ya serikali 3 ndani ya Muungano.
Na hii haikuwa ajenda ya mzee Jumbe ni shinikizo la viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama na Serikali upande wa Zanzibar.
Hivyo walijenga mikakati ya pamoja kutetea hoja hiyo kama viongozi wa upande mmoja mwanachama wa Muungano wa serikali mbili. (Tanganyika na Zanzibar)
Wakati huo Maalim alikuwa Waziri wa Elimu Zanzibar na mjumbe wa Kamati kuu ya CCM.
Hamad Rashid alikuwa Naibu Waziri wa Fedha kwenye Serikali ya Muungano na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Shabani Khamisi Mloo alikuwa mjumbe wa kamati kuu, Soud Yusuf Mgeni alikuwa mjumbe wa Halmashauri kuu.
Wote walikuwa viongozi Powerful ndani ya CCM.
Walipofika Dodoma mzigo wote walimuachia Jumbe na Waziri kiongozi wake Ramadhani Haji Fakhi.
Wajumbe wa Zanzibar waliulizwa mmoja mmoja kama kuna anayeunga mkono hoja ya serikali tatu iliyofikishwa mezani na mzee Jumbe.
Wajumbe wote wa Zanzibar walimkana ila mmoja tu, Ramadhani Haji Fakhi.
Huyu Ramadhani Fakhi aliulizwa ndani ya kikao hicho 1+1= ni ngapi?
Waliokuwa kwenye kikao hicho wanasema jamaa alishikilia msimamo wake.
Hatimaye mzee Jumbe alifutwa uanachama wa CCM na hivyo kupoteza sifa za uongozi wa serikali.
Ramadhani Fakhi alijiuzulu, ingawa baadaye kulikuwa na madai kuwa alishinikizwa kujiuzulu.
Lakini cha kushangaza mwaka 1988, watu wale wale walikuja na hoja ile ile ndani ya vikao vile vile vya CCM.
Inawezekana walikuwa na nia njema, ikiwa ndiyo hivyo kwa nini hawakuunga mkono hoja ya mzee Jumbe miaka minne nyuma?
CCM iliwatimua uanachma.