Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwaka 1972 nina miaka 28 dah!
kama ni kweli itanibidi nikupe heshima yako, umemzidi baba yangu kwa takribani miaka 17.
na kama ingelikuwa unatokea kwenye familia ya baba yangu huenda ungelikuwa ni wa kwanza au wa pili kuzaliwa.

dah humu ndani unaweza kumtukana mwanadamu anayelingana au kumzidi mzazi wako
 
Kwakweli tukio hilo nimeliona,
ingawa nilikuwa mdogo lakini lingali linapita akilini mwangu.
Nilimshangaa sana Maalim kwa kosa lile la kiufundi ambalo amefanya wakati ule.
Nadhani mpaka anafariki lazima naye alikuwa anajutia
lilikuwa ni kosa la kiufundi pindi hasira na fitina zinapokwenda zake ila unakuwa ni uamuzi sahihi kwa nyakati zile kwa sababu kila mmoja alikuwa anapigania uhai wake, ushawishi wake kisiasa na tonge yake.

ni sawa sawa na vita ya membe dhidi ya lowassa, ndio imetuletea bwana magufuli.
wangetulizana na kuaminiana huyu mtu asingeli wasokota watu wote.
wastahafu wana washwa washwa

tusisahau uamuzi ule ndio umemuinua zaidi seif na wenzake
 
1614540872852.png
 
BURIANI KAKA YANGU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD.
SEHEMU YA NNE: KUCHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA TAIFA NA MAALIM SEIF KATIBU MKUU WA CUF
Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, 28 Februari 2021

Niliporejea nchini mwaka 1998 kutoka Helsinki niliendelea na shughuli za utafiti na ushauri wa mambo ya uchumi nchi za nje. Miongoni mwa shughuli nilizofanya ilikuwa ni pamoja na kwenda Swaziland kuishauri Wizara ya Fedha ya nchi hiyo namna ya kuimarisha sera zake, kwa lengo la kukuza uchumi na kuwa na utulivu katika uchumi mpana. Aidha nilifanya ushauri kama huo kwa Wizara ya Fedha, nchini Namibia.
 
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa lina kitengo kinachoandaa taarifa ya kila mwaka ya Maendeleo ya Watu (Human Development Report). Niliteuliwa kushiriki katika maandalizi ya taarifa ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 1999 iliyojikita katika suala la Utandawazi na Maendeleo ya Watu – Globalization With a Human Face. Nilifanya utafiti na kuandaa mada kuhusu Utandawazi na Maendeleo ya nchi za Kiafrika – Globalization and Economic Development of African Countries. Nilikwenda New York kushiriki katika vikao vya kuandaa taarifa hii.
 
Back
Top Bottom