Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uamuzi ule umemkandamiza zaidi Seifu kuliko unavyofikiria.
Maalim Seif, Shaaban Hamis Mloo, Soud Yusuf Mgeni, Hamad Rashid Mohamed walikuwa na nguvu kubwa ndani ya CCM kuliko unavyodhani.
Istoshe wao pia walihusika kutoa shinikizo kwa Makamo Mwenyekiti wa CCM (Jumbe) wakadai serikali tatu kwenye vikao vya Halmashauri kuu, lakini wote walikuja kumkana mbele ya wajumbe.
Miaka minne baadaye 1988, akaleta hoja ile ile.
Tangu hapo wenye akili timamu walizijua rangi zake halisi
 
ahsante sana, sikuwa nayafahamu hayo.
kwa tafsiri yako ni kwamba walimsaliti na kumkomoa mzee jumbe
 
Katika hali hii niliamua bora nisigombee nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, na badala yake niendelee na shughuli zangu za utafiti na ushauri. Niliandika barua kwa Katibu Mkuu kuwa sintagombea nafasi ya uenyekiti wa Taifa. Chama kilituma ujumbe wa watu watatu kuja kuzungumza na mimi, ukiongozwa na Marehemu Ali Haji Pandu. Wajumbe wengine walikuwa Wilfred Lwakatare na Mzee Mbelwa. Walikuja nyumbani kwangu Sinza kunisihi nigombee nafasi ya Uenyekiti. Nakumbuka Lwakatare alitumia ‘gia’ ya kuwa ‘alau ukae kwa miezi sita ili tujipange’. Niliwaomba wanipe muda ili niweze kutafakari.
 
Hatimaye nilikubali kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa. Mzee Mloo na Maalim Seif walibadilishana nafasi. Mzee Mloo aligombea wadhifa wa Makamo Mwenyekiti, na Maalim Seif wadhifa wa Katibu Mkuu.
Baada ya Uchaguzi wa Chama wa mwaka 1999, nilianza ziara ya kutembelea mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar. Mzee Mloo alishauri nianze ziara mikoa ya kusini.
 
Nilianza ziara Mkoa wa Lindi. Hata hivyo mikutano yangu ya hadhara iliwekewa vizingiti vingi. Tarehe 31 Desemba 1999 nilipokuwa Lindi Mkutano wangu wa hadhara uliokuwa umepangwa kufanyika jioni ulizuiliwa na polisi kwa kisingizio kuwa wananchi wa Lindi walikuwa wanajiandaa na sherehe za mwaka mpya na kuipokea karne ya 21! Tulipoteza siku nzima katika mazungumzo na hatimaye aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, mtani wangu, Marehemu Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, aliwaeleza Polisi wasizuie Mkutano. Tulianza kutangaza mkutano huo saa 9 alasiri na kufanya mkutano saa 11 jioni.
 
Newala tulizuiliwa kufanya Mkutano wa hadhara kwa kisingizio kuwa Taarifa ya mkutano imewafikia Polisi chini ya saa 48 kabla ya tukio. Tuliamua tufanye mkutano wa ndani. Tulikodi Ukumbi wa Chuo. Gari ya matangazo ilipoanza kutangaza mkutano wa ndani, ilizuiwa na polisi na kuelezwa kuwa mkutano wa ndani hautangazwi kwa kipaza sauti! Afisa Mfawidhi (OCD) wa Polisi alitueleza kuwa taarifa ya mkutano wa ndani inapaswa kupelekwa kwa wahusika kwa barua na siyo kwa kuwatangazia kwa kipaza sauti. Kwa sababu ya hivyo visingizio hatukuweza kufanya huo mkutano wa ndani.
 
Mkutano wetu Mtwara mjini uliokuwa ufanyike tarehe 10 Januari 2000, ulizuiliwa na Polisi kwa kisingizio kuwa katika wiki ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, majeshi yote yalikuwa 'standby'. Nilipomuona Mkuu wa Mkoa, Nsa Kaisi, anisaidie alinijibu kuwa yeye hana madaraka juu ya Polisi Mkoani kwake. Alinieleza kwamba anayeweza kuingilia kati ni IGP na maafisa wa juu wa makao makuu ya polisi. Alinieleza kuwa Mtwara ilikuwa na matatizo ya kiusalama kwani haikuwa inawezekana kutofautisha kati ya Mmakonde au Mmakua wa Msumbiji, na Mmakonde au Mmakua wa Tanzania! Utadhani Msumbiji na Tanzania hazikuwa nchi marafiki.
Wakati tunazuiwa kufanya mikutano ya hadhara mkoani Mtwara, Mzee John Malecela, Makamo Mwenyekiti wa CCM, alikuwa anafanya mikutano ya hadhara mkoani Tabora.
 
Nilitembelea mikoa yote ya Tanzania isipokuwa Rukwa. Sikuweza kutembelea Rukwa kwani nilipofika Kigoma Julai 2000, Polisi walianza kuzuia mikutano ya hadhara kwa kisingizio kuwa kampeni hazijaanza pamoja na kwamba sheria namba 5 ya Vyama vya Siasa ya 1992, haizuwii kufanyika mikutano ya vyama muda wowote ule, kwa ajili ya kuelezea sera za chama na kusaka wanachama wapya. Nadhani hofu kuu ya CCM ilikuwa ni kuona jinsi Wananchi wa Tanzania walivyokuwa wanaitikia kaulimbiu ya CUF ya Haki Sawa kwa Wananchi wote, na nia yetu ya dhati ya kujenga uchumi imara utakaoleta neema kwa wote. CUF ilikuwa tishio katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000.
 
ahsante sana, sikuwa nayafahamu hayo.
kwa tafsiri yako ni kwamba walimsaliti na kumkomoa mzee jumbe
Chanzo cha yote ilikuwa ni madai ya msingi ya
Wazanzibar.
Walikuwa na vikao Afisi kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar.
Walishambuliana hatimaye walikubaliana waende Dodoma wakiwa na madai ya serikali 3 ndani ya Muungano.
Na hii haikuwa ajenda ya mzee Jumbe ni shinikizo la viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama na Serikali upande wa Zanzibar.

Hivyo walijenga mikakati ya pamoja kutetea hoja hiyo kama viongozi wa upande mmoja mwanachama wa Muungano wa serikali mbili. (Tanganyika na Zanzibar)
Wakati huo Maalim alikuwa Waziri wa Elimu Zanzibar na mjumbe wa Kamati kuu ya CCM.
Hamad Rashid alikuwa Naibu Waziri wa Fedha kwenye Serikali ya Muungano na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Shabani Khamisi Mloo alikuwa mjumbe wa kamati kuu, Soud Yusuf Mgeni alikuwa mjumbe wa Halmashauri kuu.
Wote walikuwa viongozi Powerful ndani ya CCM.

Walipofika Dodoma mzigo wote walimuachia Jumbe na Waziri kiongozi wake Ramadhani Haji Fakhi.
Wajumbe wa Zanzibar waliulizwa mmoja mmoja kama kuna anayeunga mkono hoja ya serikali tatu iliyofikishwa mezani na mzee Jumbe.
Wajumbe wote wa Zanzibar walimkana ila mmoja tu, Ramadhani Haji Fakhi.
Huyu Ramadhani Fakhi aliulizwa ndani ya kikao hicho 1+1= ni ngapi?
Waliokuwa kwenye kikao hicho wanasema jamaa alishikilia msimamo wake.
Hatimaye mzee Jumbe alifutwa uanachama wa CCM na hivyo kupoteza sifa za uongozi wa serikali.
Ramadhani Fakhi alijiuzulu, ingawa baadaye kulikuwa na madai kuwa alishinikizwa kujiuzulu.
Lakini cha kushangaza mwaka 1988, watu wale wale walikuja na hoja ile ile ndani ya vikao vile vile vya CCM.
Inawezekana walikuwa na nia njema, ikiwa ndiyo hivyo kwa nini hawakuunga mkono hoja ya mzee Jumbe miaka minne nyuma?
CCM iliwatimua uanachma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…