Kwa mujibu wa taarifa ya BBC ya April 14, 2018 ni kwamba miaka ya 1960 John alipata kazi ya ualimu katika shule moja ya upili huko New Mexico lakini baadae akafichua siri kwamba licha ya kuhudumu kama mwalimu kwa miaka 17 lakini hakua anajua kusoma wala kuandika.
"Nilichelewa sana kuzungumza, katika miaka 6 ya kwanza ya maisha yangu sikua bado nna uwezo wa kuzungumza, wazazi wangu wakanipeleka shule hivyo hivyo na kuniambia mimi ni mshindi"
"Katika mwaka wa kwanza shuleni hali ilikuwa sawa, hakukuwa na chochote zaidi ya kusimama kwenye mstari, kukaa chini, kwenda bafuni kuoga na kulala"
"Mwaka wa pili tulitakiwa kujifunza kusoma na kuandika lakini kwangu ilikuwa ni kama kufungua gazeti la kichina, sikuelewa chochote, mpaka nafikisha miaka nane nilikuwa mtoto ambaye siwezi hata kueleza shida kwa mtu"
"Wakati mwingine nilikua naamka usiku na kusali kuwa Mungu anisaidie kusoma, kisha naamka tena kufunua kitabu labda nitaona muujiza lakini sikupata muujiza huo"
"Shuleni niliishia kua bubu, sikujua hata ninasemaje kuomba nitoke nje, sikujua hata nilifikaje hapo, sikuwa hata swali gani la kuuliza"
John anasimuliza zaidi na kusema alipata kazi ya ualimu wa shule ya upili kwa njia za panya mwaka 1961 na akafundisha kwa miaka 17 mpaka 1978 huku akiwa hajui kusoma wala kuandika. Anasema alikuwa anafundisha wanafunzi kuwa watafutaji na alikuwa muongo mkubwa.
Alianza kujifunza kusoma na kuandika akiwa na miaka 48 miaka ya 1980 baada ya kuacha kazi hiyo miaka 8 nyuma na baadae kuamua kuitoa siri yake hiyo.