Tafiti: Kampuni mbili, Xtera na KDDI Research wamerekodi kasi ya Intaneti iliyofikia 178TPBS (Terabits per second). Kwa kasi hiyo unaweza kushusha filamu na series' zote kwenye Netflix chini ya sekunde moja tu.
Jonas Salk' baada ya kugundua chanjo ya ugonjwa wa Polio' aligoma kuiwekea hatimiliki yake ili kujipatia fedha na faida nyingine kama makampuni mengi ya dawa yanavyofanya. Alipoulizwa kwanini alisema " “Siwezi kuiwekea hatimiliki, Je Waweza kuliwekea hatimiliki Jua?."
Siku 1 utayokaa kwenye sayari ya Zebaki (Mercury) ni sawa na siku 176 kwa Dunia, Lakini Siku 88 kwenye sayari ya Mercury ni sawa na mwaka 1 kwa Dunia. Maana yake ni, Sayari ya Mercury inatumia muda mfupi zaidi kulizunguka jua kuliko kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake.
"The Necronomicon" ni kitabu kinachotajwa kuwa cha kishetani au mizimu kilichoandikwa miaka 800 iliyopita. Unaambiwa vitu ulivyosoma hukutokea ukweli kihisia, Inatajwa mmoja kati ya watu walioandika kitabu hicho hakua mtu wa kawaida bali "Jini", Waandishi wengi wanaojaribu kukitafsiri hugeuka vichaa.
Familia ya 'Rothschild' inatajwa kama moja ya familia tajiri zaidi kuwahi kutokea katika historia ya ulimwenguni licha ya vitu vingi ambavyo vinawapa utajiri haviwekwi sana wazi na hata familia nzima tangu enzi mpaka sasa maisha yao ni ya usiri sana. Kwa mujibu wa data za mwaka 2020, thamani ya utajiri wao inakadiriwa kufikia Tsh Trilioni 927
Tegemea ujio mpya wa Sneaker' kutoka kwa Kanye West mwezi Machi, 2021, Ambapo zinatarajiwa kuanza kupatikana mtandaoni bila makato ya kodi kwa Tsh 463,525/=
Kupumua kwa njia ya haja kubwa (Kujamba) kunaweza kusababisha madhara mpaka ugonjwa kwa watu wengine kama mtu anaefanya kitendo hicho (Mjambaji) atakua Uchi lakini akivaa nguo inatajwa kutokua na madhara.
Tafiti: Wanaume ambao wana kipato kidogo cha fedha huvutiwa zaidi na Wanawake wenye matiti makubwa wakati Wale ambao wana kipato kikubwa hupendelea Wanawake wenye matiti madogo.Chanzo: Metro
Felix Batista, FBI kutoka Marekani alikuwa akiwafundisha watu namna ya kujikinga na kutekwa nchini Mexico. Disemba 10 mwaka 2008 baada ya kutoka kufundisha alitekwa na hadi leo hajapatikana.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.