NJIA NZURI YA KULIPA KISASI
i/Tabasamu-Tabasamu ni pambo zuri kuliko pambo lolote miongoni mwa mapambo yote duniani.Huipamba sura ya binaadamu na kuficha maumivu,sononeko na hata maswahibu uliyo wahi kukumbana nayo.Tabasamu humuumiza aliyekuwa na nia mbaya kukutenganisha na tabasamu lako la asili.Mara nyingi mtu akikufanyia ubaya,huwa na nia mbaya kukuumiza kisaikolojia,lakini kitendo cha kutabasamu humfanya mbaya wako kujiona kuwa kashindwa kutimiza lengo lake na hali hiyo huumiza sana moyoni mwake.