Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hugo Chaves
Che Guevara
Fidel Castrol
Lao moja hawa. Makomredi walioamini kabisa kabisa katika itikadi na falsafa zao za kiMarx. Japo juhudi zao pengine hazikufanikiwa lakini miamba hawa ni mifano bora kabisa ya watu ambao angalau waliweza kusimama imara na kupambana na mfumo wa kibeberu kwa vitendo - huku ama wakiuawa au kukoswa koswa kuuliwa na mabeberu hao kwa zaidi ya mara elfu. Elcommandantes....
 
IDD Amin Dada
Samuel Doe
Benito Mussolini
Maoze Dong
Lao moja hawa. Wakiwemo madikteta wa kutisha walioua mamilioni ya watu japo baadhi yao hawakuumaliza mwendo salama. Mmoja wao aliuliwa kama jambazi akakatwa uume na masikio yake kisha akafungwa kwenye difenda ya jeshi na kuanza kuburutwa kama mbwa mitaani huku umma ukishangilia. Madaraka na wajibu - dhana tata lakini zinazopaswa kukamilishana...
 
Yasser Arafat
Lao moja. Wote walitaka kuwakomboa watu wao. Naam! Gaidi wako anaweza kuwa shujaa wangu (ende vaisi vesa). Mmoja hapo alipachikwa ugaidi japo kwa watu wake alikuwa mpigania uhuru na kiongozi mtegemewa. Wote waliishia kuuawa - mmoja kwa kupigwa risasi kwa kutishia madaraka ya mwenzake na mwingine kwa kunyweshwa sumu....Haki na uhuru. Vigumu sana kuvipata kwa binadamu aliyejijengea jamii yenye matabaka yenye kunyonyana na kukengeushana!
 
Lao moja hawa. Wakiwemo madikteta wa kutisha walioua mamilioni ya watu japo baadhi yao hawakuumaliza mwendo salama. Mmoja wao aliuliwa kama jambazi akakatwa uume na masikio yake kisha akafungwa kwenye difenda ya jeshi na kuanza kuburutwa kama mbwa mitaani huku umma ukishangilia. Madaraka na wajibu - dhana tata lakini zinazopaswa kukamilishana...
Nikweli mpendwa
 
Lao moja. Wote walitaka kuwakomboa watu wao. Naam! Gaidi wako anaweza kuwa shujaa wangu (ende vaisi vesa). Mmoja hapo alipachikwa ugaidi japo owa watu wake alikuwa mpigania uhuru na kiongozi mtegemewa. Wote waliishia kuuawa - mmoja kwa kupigwa risasi kwa kutishia madaraka ya mwenzake na mwingine kwa kunyweshwa sumu....Haki na uhuru. Vigumu sana kuvipata kwa binadamu aliyejijengea jamii yenye matabaka yenye kunyonyana na kukengeushana!
Ni nani kati hao wawili huyu Malcom X ninavyofahamu alikuwa mwanaharakati aliyepinga ubaguzi wa rangi.
 
Mungu Ibariki Afrika
Wabariki viongozi wake
Hekima umoja na amani
Muuungu Ibariki
Afrika na watu wake.....

Screenshot_20210304-214517_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom