(Mteja A na Muuzaji A)
Mteja A: “Habari, kuna losheni ya kuondoa chunusi?”
Muuzaji A: “Ipo ya Aloe Vera shilingi elfu tano, nikupe ngapi?”
(Mteja A na Muuzaji B)
Mteja A: “Habari, kuna losheni ya kuondoa chunusi?”
Muuzaji B: “Ndio ipo, unataka ya wanaume au ya wanawake?”
Mteja A: “Ya wanawake”
Muuzaji B: “Ipo ya Aloe Vera ile OG, hii inaondoa chunusi na haichubui ngozi kabisa, tena nitakushauri jinsi ya kuichanganya ili ikubali zaidi ngozi yako.”
Mteja A: “Unauzaje?”
Muuzaji B: “Moja ni shilingi elfu tano, ila ninaweza kukupunguzia kidogo….ukinunua nyingi pia nitakupunguzia zaidi.”