Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kutazama hayo mazungumzo hapo juu unafikiri mteja A atanunua losheni kwa muuzaji A au B? Ni wazi kuwa atanunua kwa muuzaji B kwa sababu anajua kunadi bidhaa yake vyema kwa kuhakikisha mteja anapata maelezo ya kutosha ya bidhaa na bei.
 
Fahamu vyema huduma na bidhaa unazouza, haifai mteja kuja kwako na kukuuliza kuhusu huduma au bidhaa zako ukashindwa kumpa maelezo ya kuridhisha. Kumbuka kuwa wateja watafiti wanataka kupata maelezo ya kina kabla hawajafanya manunuzi.
 
Wateja wapitaji
Hawa ni wateja ambao huja kwenye biashara yako mara moja tu, na si rahisi kuja tena mara nyingine au karibuni. Mara nyingi wateja wa aina hii huwa ni wasafiri au watu walioletwa kwenye eneo lako la biashara kutokana na tukio fulani kama vile msiba au sherehe
 
Ingawa wateja hawa ni wapitaji, unapaswa kuwahudumia vyema kwani hujui kesho itakuwaje. Ili kuwapata wateja hawa ni vizuri kujenga jina jema katika eneo husika ili mteja mgeni afikapo katika eneo unalofanyia biashara akubaini wewe kwanza kabla ya kumbaini mfanyabiashara mwingine
 
Wateja walalamikaji
Hii ni aina ya wateja ambao wanapenda kulalamika na kulaumu sana. Si rahisi kuwaridhisha wateja hawa kwani wao kila kitu kwao ni tatizo. Hata hivyo, pamoja na tabia yao hii, bado utaendelea kuwaona wakija kila mara
 
Ukimpunguzia bei atasema ni mbinu ya kumvuta umuibie, ukimweleza ubora wa bidhaa atakuambia unamrubuni ili anunue, ukimwambia bei za vitu zimepanda atakuambia unamdanganya…n.k. Wateja hawa kamwe huwezi kuwaridhisha kwani kila mara huona kuwa mfanyabiashara si mwaminifu au anapata faida kubwa sana kwa ujanja ujanja.
 
Wateja wasiokuwa na mpango wa manunuzi
Je umewahi kununua kitu sokoni au dukani ambacho hakikuwa kwenye mpango wako wa manunuzi kwa kuwa tu umekiona au mtu mwingine amekushawishi kukinunua? Au umewahi kusikia mtu akisema nimenunua hiki kitu kwa sababu nimekuta kinauzwa bei nzuri nikaona nisikiache?
 
Ikiwa jibu ni ndio, wewe au huyo mtu mwingine wote mlikuwa wateja wasiokuwa na mpango wa manunuzi. Wateja hawa hufanya manunuzi ambayo hawakuyapanga awali; mara nyingi hufanya manunuzi kutokana na tamaa ya macho au ushawishi wa marafiki au muuzaji.
 
Wateja wanaotafuta ubora
Kutokana na hali ya ugumu wa maisha, wateja wa aina hii ni wachache sana. Wateja wanaotafuta ubora ni aina ya wateja ambao wao hawaoni shida kutumia gharama kubwa kutafuta bidhaa yenye ubora wanaouhitaji.
 
Je, umewahi kujiuliza inakuwaje mtu anaacha kiatu cha ngozi cha shilingi 50,000 na kwenda kununua kiatu cha ngozi cha Italia chenye thamani ya zaidi ya shilingi 650,000? Hii ni kutokana na sababu kuwa mteja huyu anataka ubora wa bidhaa yake.
 
Ikiwa unataka kuwapata wateja wa aina hii, basi zingatia kuweka bidhaa za bei tofautitofauti kwenye biashara yako. Kumbuka, bidhaa za bei ghali zinatakiwa kuwepo kwa uchache na baada ya kufanya tathimini kubwa kwani mzunguko wake ni mdogo sana kutokana na uchache wa wateja wake
 
Back
Top Bottom