Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwaka 2016 Julio Macias Gonzalez Kijana wa miaka 17 raia wa Mexico alifariki baada ya kupigwa Love Bite na mpenzi wake. Baada ya uchunguzi Madaktari walisema kitendo hicho kilipelekea damu kusafiri hadi kwenye ubongo. Wazazi wa kijana huyu walitupa lawama zote kwa binti aliyekua mpenzi wa mtoto wao ambaye baada ya tukio ilo inaaminika aliwekwa mafichoni kwaajili ya usalama wake. Pia wazazi walieleza kuwa mara kadhaa walishawahi kumkataza kijana wao kuwa na uhusiano na binti huyo ambaye alikua na miaka 24, miaka 7 zaidi ya Julio lakini hakuskia. Ukiachana na hii kesi ya Julio, Mwaka 2010 mwanamke wa miaka 44 kutoka New Zealand aliripotiwa kudhulika kwasababu hii pia. Wazee wa maLove bite kuweni makini aisee
 
Florence Irene Ford alifariki akiwa na umri wa miaka 10, Wakati wa mazishi Mama yake alifanya ombi la kushangaza, aliomba jeneza la binti yake liwekewe dirisha dogo na ngazi kaburini kuelekea chini kwenye jeneza. Kabla ya kufariki, Florence, aliyezaliwa Septemba 3, 1861, alikuwa anaogopa sana dhoruba. Mara tu kukiwa na dhoruba, alikuwa akimkimbilia mama yake, ambaye alimfariji kwa kumkumbatia hadi dhoruba hiyo ipite. Mwaka 1871, akiwa na umri wa miaka 10, Florence alikufa kwa homa ya manjano. Mama yake akiwa amefadhaika, alitamani mwanae asizikwe, kwani bado alikuwa anataka kumfariji wakati wa dhoruba, hata alipokuwa amekufa.
 
Aaron Chervenak mwanaume kutokea Las Vegas, Marekani mwenye umri wa miaka 39 kwa sasa. Mwaka 2016 alisafiri kutokea Las Vegas mpaka Nevada katika ukumbi wa sherehe wa The Little Vegas Chapel ili kufunga ndoa na simu yake ya mkononi(smartphone). Aaron alisema kuwa alipofika tuu mjini Nevada aliwasiliana na moja ya makanisa yaliyopo mjini hapo ili kuona kama yatakubali kufungisha ndoa yake hiyo isiyo ya kawaida, na alifurahi sana baada ya kuona ilikuwa rahisi kwake kukubaliwa. Simu yake hiyo aina ya iphone ilionekana ikiwa imevalishwa kava (cover) jeupe na ikasimamishwa kwenye stand ndogo maalumu kwa simu na kuwekwa karibu naye mbele ya kanisa. Kulikuwa na wageni wachache tuu waliohudhuria ndoa hiyo japo baadae uongozi wa kanisa wa jimbo la Nevada ulisema kuwa hawaitambui ndoa hiyo. Wakati wa ndoa hiyo kanisani hapo mfungishaji alisema kuwa anamtakia Aaron furaha na nyakati nzuri katika ndoa yake hiyo akiwa na simu yake kama mkewe, na baadae akamuuliza mbele ya kanisa kama anaahidi kumheshimu na kumfariji mkewe huyo, Aaron akasema Ndio. Ulipofika wakati wa kuvishana pete Aaron alichukua simu yake na kuingiza kidole chake ndani ya pete ambayo ilikuwa imeunganishwa na kava (cover) la simu hiyo kumaanisha kuwa simu hiyo ilikuwa imemvisha pete bwana Aaron. Baada ya ndoa Aaron alimbeba mkewe huyo huku akionekana mwenye furaha akitoka kanisani.
 
Nadia Matievskaia ni raia wa Minsk, Belarus, anatimiza umri wa miaka 23 mwaka huu, amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na ubunifu wake katika sanaa ya uchoraji. Bibie huyu Ni mchoraji maarufu ambae anachora kwa kutumia Matiti. Hapo awali hakuwahi kufikiria kama atakuja kuwa mchoraji mkubwa kiasi alichofikia. Ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwa Mwanamuziki na baadae alikuja kugundua kuwa ana kipaji kingine cha kuchora. Ajabu zaidi hatumii mikono kuchora, anatumia chuchu za matiti yake, anachovya rangi na kuchora . . Nadia anasema kuwa hajawahi kuingia darasani kusomea fani hii ya uchoraji, na imekuwa ni kazi inayomuingizia pesa nyingi kwakua anachora picha nyingi kwa namna hiyo na kuziuza kwa watu mbalimbali.
 
teknolojia ya kuhifadhi miili ya watu waliokufa, inahifadhi mwili kwenye kiwango cha baridi kali sana ili usiweze kuharibika kwa matumaini kwamba ipo siku moja watafufuliwa. Hatua za kuhifadhi mwili kwa ajili ya kuufufua baadae huanza ndani ya dakika chache baada ya moyo kusimama kwa kuuhifadhi kwenye baridi kali na kutumia kemikali ambazo zinazuia mwili huo kutoharibiwa na barafu. Wataalamu wanaamini mtu anaweza kukaa humo miaka milioni 24 bila kuharibika Kwa teknolojia iliyopo sasa uwezo wa kuamsha wafu hao bado haupo lakini wataalamu wanaamini miaka ijayo kitu hicho kitawezekana. Wataalamu wa cyronics wanaamini watu waliohifadhiwa watakuja kufufuliwa na teknolojia ya hali ya juu miaka 100 mpaka 500 ijayo kutokana na kukua kwa fani za bioengeneering, nanotechnology na nanomedicine. Mtu anayehifadhiwa akiwa na miaka 15 baada ya miaka 100 au miaka 200 mbele atakua na umri ulele wa miaka 15 yaani bado kijana. Wataalamu walioanzisha teknolojia hii wanaamini kwamba kifo ni hatua fulani ya maisha ambayo mtu anapitia kabla ya kufika mwisho wa maisha hivyo hatua hii inaweza kuzuiliwa. Mpaka mwaka 2014 gharama ya kuhifadhi mwili wa mtu anayehitaji ilikua milion 400 za kitanzania kwa kipindi chote utakachohifadhiwa pamoja na ghrama ya kufufuliwa. Kwa sasa teknolojia hii ipo nchi mbalimbali zilizoendelea kama marekani, urusi,canada, ufaransa na kadhalika. Dr.james bedford alikua binadamu wa kwanza kuhifadhiwa mwaka 1967 na mpaka mwaka 2014 miili 250 ilikua imehifadhiwa nchini marekani huku zaidi ya watu 1500 wakijiandikisha kuhifadhiwa siku wakifa pia.
 
IMG-20210314-WA0002.jpg
 
Mwaka 2019 huko Madrid, Hispania kijana mwenye umri wa miaka 26 aliyefahamika kwa jina la Alberto Sánchez Gomez alikamatwa na Polisi kwa kosa la kumuua mama yake mzazi María Soledad Gómez aliyekua na miaka 66. Uchunguzi wa Polisi ulianza baada ya mama huyo kutoonekana mwezi mzima. Polisi walifika nyumbani kwake kwaajili ya kuchunguza baada ya kupewa taarifa na majirani, walipofika walikuta nyama nyingi chumbani kwa Alberto. Polisi walipofanya uchunguzi waligundua kuwa nyama ile ni ya binadamu. Baada ya kukamatwa Alberto alikiri kuwa ni kweli alimuuwa mama yake, akamkatakata vipande na kuanza kula nyama akisaidiana na mbwa wake. Ripoti ya polisi ilisema kuwa Alberto alikuwa mtumiaji mkubwa wa dawa za kulevya
 
Mwaka 2013 vyombo mbalimbali vya habari kama CNN na mtandao wa the sun wa uingereza viliripoti taarifa ya mwanamke raia wa Australia aliyefariki baada ya kushambuliwa na jogoo bandani alipoenda kukusanya mayai ya kuku wake. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 76 ambae jina lake halikuwekwa wazi alishambuliwa na Jogoo mguuni na kusababisha damu nyingi kumtoka na kupelekea kifo chake.
 
Muimbaji nyota raia wa Colombia Shakira Isabel Mebarak Ripoll, maarufu kwa jina la SHAKIRA, mwaka 2010 alitoa wimbo kwaajili ya kombe la dunia alioupa jina la "Wakawaka". Baada ya Shakira kuachia wimbo huo alishtakiwa na kundi la Golden Sound kutokea Cameroon kwa kuiba wimbo wao "Zangalewa" ambao ulitoka mwaka 1986.
 
Antoine-Augustin Parmentier, alikuwa ni mfamasia wa ufaransa. Wakati alipokuwa akihudumu kama mfamasia wa jeshi la Ufaransa, kipindi iko wakati wa vita kati ya Ufaransa na Prussia, alikamatwa na jeshi la Prussia na akawa analishwa viazi tu wakati wote wa kifungo chake. Wakati huo nchi yake ya Ufaransa ilikuwa imekataza kilimo cha viazi na kipindi iko viazi vilikuwa chakula cha nguruwe. Alinusurika na kutoka mikononi mwa Prussia, akiwa mwenye afya na umbo zuri lililojengeka. Baada ya kurudi kwao alianza kuwashawishi viongozi na wananchi kula viazi na kuwaelezea sifa za viazi. Kutokana na bidii yake, Ufaransa ilitangaza viazi kuwa chakula cha binadamu mwaka 1772. Kaburi lake huko Paris limepambwa na mimea ya viazi kama njia ya kumuenzi.
 
Siku moja vipofu wawili walikua wanapigana. Ghafla umati wa watu uliwazunguka. Baadhi ya watu walijaribu kuwaachanisha wasipigane lakini vipofu wale hawakusikia ndo kwanza waliendelea kupigana. Mtu mmoja kutoka kwenye umati wa watu wale akalopoka kwa sauti " Waacheni wapigane, Mimi na bet elfu 10 kwa yule aliyeshika kisu ndo atashinda." vipofu kuskia hivyo ghafla wote wawili wakakimbia.😂😂😂
 
Mwaka 1935, wavuvi walimkamata Papa na kumuweka kwenye bwawa la kioo kwaajili ya maonesho huko Sydney, muda mfupi baada ya kumuweka humo alitapika mkono wa binadamu. Mtaalam wa Papa alithibitisha kuwa Papa hakuwa ameukata mkono huo kwa meno yake, bali mkono huo ulikuwa unaonekana umekatwa kwa panga. Mkono huo pia ulikuwa na tatoo, ambayo ilifahamika kuwa ni ya mtu ambaye aliripotiwa kupotea wiki chache zilizopita. Tukio ili liliibua na kusababisha uchunguzi wa kesi ya mauaji na hatimaye kukamatwa kwa wahalifu.
 
Huko Nyanda za juu, Papua New Guinea zamani kuliishi kabila la watu wanaoitwa Fore. Fore walikuwa hawajawahi kuchangamana na watu kutoka sehemu nyingine hadi kufikia miaka ya 1930 Wakati watafiti walipokwenda katika kijiji chao. Fore walikua wanakula wafu wao (ndugu zao waliokufa) badala ya kuwazika ili kuwakinga wasiliwe na minyoo na funza. Ilikua ni kama ishara ya kuonesha upendo kwao. Fore walikumbwa na ugonjwa wa ajabu "laughing death" (kifo cha kucheka) uliokua ukiua watu wengi sana hususani wanawake na watoto . Ugonjwa huo uliitwa KURU. Kuru ni ugonjwa unaotokana na kula ubongo wa binadamu. Takribani nusu karne ilipita tangu watu wa Fore walipoacha kula wafu wao lakini janga hilo liliendelea kudumu hadi mwaka 2012 watafiti walipotangaza kuisha kwa ugonjwa huo. Mwathiriwa wa mwisho wa kuru alikufa mwaka 2009.
 
Valentina kutokea Russia ndiye mwanamke anaeshikilia rekodi ya dunia ya mwanamke aliyezaa watoto wengi zaidi akiwa na mwanaume mmoja tu, mumewe Feodor Vassilyev. Valentina na mumewe walizaa jumla ya watoto 69 👉 jozi kumi na sita za mapacha (mapacha wawili wawili mara 16 ambao ni jumla ya watoto 32), 👉seti saba za mapacha watatu (mapacha watatu mara 7 ambao ni jumla ya watoto 21) na 👉seti nne za mapacha wanne (mapacha wanne mara 4 ambao jumla 16). Ni sawa na kusema alizaa mara 27. Watoto hawa wote aliwazaa kwa miaka 40 tu, kuanzia miaka ya 1725 hadi 1765. Ukiachana na watoto hao 69, inadaiwa Feodor Vassilyev (mume wa Valentina) pia alikuwa na watoto wengine 18 ambao alizaa na mke wake wa pili. Hivyo Feodor Vassilyev jumla alizaa watoto 87.
 
Imani hii inaitwa Reincarnation (Kuzaliwa upya), ni imani ambayo ipo tangu miaka mingi sana, zaidi ya miaka 1000 iliyopita na bado inaaminika hadi sasa. Reincarnation ni neno la kilatin lenye maana ya "entering the flesh again", yaani kitu kile kile lakini kinaingia sehemu mpya. Miongoni mwa watu wenye imani hii ni watu wa dini za Kihindu (Hinduism),Budha (Buddhism) na Jain (Jainism). Wanaamini kuwa mtu anapokufa nafsi yake inabaki duniani na kutafuta mwili kwaajili ya kuzaliwa upya. Mtu anapozaliwa upya hakumbuki chochote kuhusu maisha yaliyopita na anaweza kuzaliwa upya akiwa katika muonekano ule ule wa kimaumbile (same physical appearance) au akazaliwa akiwa katika mwili mwingine. Inaelezwa kuwa kama ukiota kuhusu maisha tofauti na unayoishi sasa, basi ni dhahiri nafsi yako ilitumiwa na mtu kabla kwa namna hiyo, au ukienda sehemu na ukahisi umeshawahi kufika au hata kuota kuna sehemu kama hiyo, ni uthibitisho kuwa mtu mwingine aliyewahi kutumia nafsi yako alifika eneo hilo. Licha ya dini hizi kuwa na imani sawa kuhusu kuzaliwa upya, lakini zinatofautiana kuhusiana na ukomo wa idadi ya kuzaliwa upya. Kuna wanaoamini hakuna ukomo wa idadi ya kuzaliwa upya, wengine wanaamini mwisho mara 7 na wengine mara 13. Wanaoamini ukomo wa mara 13 wanaamini mtu akishazaliwa upya mara 13 ndipo nafsi yake hupotea jumla duniani, yaani ukifa basi roho yako atazaliwa nayo mtu mwingine, naye akifa itahamia kwa mwingine hadi mkifika watu 13 nayo inapotea mazima. Kulingana na imani hii kuna namna ya kujua wewe ni uzao wa ngapi wa nafsi yako. Mfano mimi nimezaliwa tarehe 18.03.1996, unajumlisha namba zote katika tarehe yangu ya kuzaliwa 1+8+0+3+1+9+9+6 unapata jumla 37. Alafu unajumlisha tena namba hizi 👉 3+7=10, Jibu unalopata ndiyo idadi ya uzao wa nafsi yako uliopo, Kwahiyo mimi ni mtu wa 10 katika uzao wa nafsi niliyonayo, nikifa atazaliwa nayo mtu mwingine wa 11 hadi ifike mwisho 13. Wanaamini kuwa binadamu anaishi mara moja, lakini roho yake inaishi maisha 13 ndipo inapotea kabisa duniani, japo inakuwa haina kumbukumbu yoyote juu ya maisha mengine ya nyuma. Pia inaaminika kwamba watu wanazaliwa upya ili kukamilisha yale waliyopanga kabla ya kufa.
 
Watu wa misri ya kale (Ancient Egyptians) waliabudu na kuheshimu sana Wanyama. Waliheshimu Wanyama kwasababu tofauti tofauti. Mbwa walithaminiwa kwa uwezo wao wa kulinda na kuwinda, lakini Paka walichukuliwa kuwa wa kipekee zaidi. Wamisri waliamini paka walikuwa viumbe wa ajabu, wenye uwezo wa kuleta bahati nzuri kwa watu wanaowafuga. Kwa kuwaheshimu wanyama hawa, familia tajiri ziliwavalisha vito vya thamani na kuwalisha vyakula vya kifalme. Jambo ambalo ni tofauti sana na maisha ya sasa, Kipindi hicho ilikuwa kama ikitokea Nyumbani Paka amekufa, watu wote wanaokaa kwenye nyumba hio wananyoa nyusi zote katika macho yao, lakini wale ambao nyumbani kwao Mbwa amekufa walikua wananyoa nywele zote mwilini hadi kichwani. Hii ilikua kama ishara ya kuomboleza na waliendelea kuomboleza hadi nywele zao zikikua. Katika kipindi hiki Paka walikuwa maalumu sana kiasi kwamba ikitokea mtu akawaua, hata kwa bahati mbaya, alihukumiwa kifo.
 
Back
Top Bottom