Kgothalo
JF-Expert Member
- Jan 6, 2015
- 8,491
- 46,839
Siasa zimeanza kukita kambi kwenye uzi huu na kuhatarisha kabisa uwepo wa huu uzi.Wadau wa uzi wa likes nawapenda sana huu ni moja wa uzi ambao tuliubatiza jina la no stress zone
Hakuna stress kwenye uzi huu unapost chochote utapata likes kasoro lugha chafu picha chafu
But now days naona siasa mnaingiza humu sio sahihi wapendwa tujiweke pembeni na siasa kwenye uzi wet pendwa
Napenda firigisi[emoji39][emoji39][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]unapenda mahindi ya kuchoma na firigisi za kukaanga? Nimekuuliza hivi unaunga mkono maovu mbali mbali dhidi ya Watanzania? Hutaki kujibu [emoji12][emoji12][emoji12]
Kitabu gani hiki sis?
Demokrasia ya kiafrika ni ya kipuuzi sana, Demokrasia yenyewe inaishia pale mtu anapodai haki yake akaipata.Demokrasia, haki na uhuru. Ni dhana tata ajabu. Japo kila mtu ana haki na uhuru wa kutenda anachotaka lakini pia ni lazima kuangalia matakwa ya wengi. Na hapo ndipo dhana ya demokrasia inaingia. Kwamba uhuru wako wa peke yako kutaka kufanya ukitakacho unaweza kuzimwa na uhuru wa wengi kama kitu unachotaka kukifanya hakiwapendezi wengi. Na huu ni msingi wa muhimu sana katika kuleta utangamano katika jamii vinginevyo kila mtu angekuwa anafanya tu anachotaka akidai kuwa ni uhuru wake haijalishi kama analolifanya linawakera wanajamii wenzake.
Na huwezi kuwa mpigania demokrasia, haki na uhuru (wa kweli) kama huheshimu maoni ya wengine - hasa ya walio wengi kwa sababu huo hasa ndiyo msingi wa demokrasia unayoipigania. Kwamba wewe ndiyo wewe, ulitakalo lazima lifanyike kwa sababu ni haki yako; na uhuru wako uko juu ya kila mtu. Hapana! Huu ni udikteta!
Tumeishi katika uzi huu kwa amani na upendo sana kwa sababu kuna misingi ambayo tulikuwa tumejiwekea. Misingi ambayo ilituepusha na chuki na ugomvi - kuepuka siasa, dini, matusi na picha za utupu. Kwa kufuata misingi hii tumejenga urafiki na undugu humu. Inaumiza kuona kuwa leo hii tunatukanana sisi kwa sisi. Ndiyo maana wengine hatuonekani sana katika uzi huu tena.
Jukwaa la siasa lipo. Jukwaa la dini lipo. Anayeyataka haya ayafuate huko na akaporomoshe matusi yake huko; apate na ban yake huko. Mtuachie kijiwe chetu hiki cha upendo tuendelee kucheka na kufurahi. Vinginevyo bakini na uzi wenu !!!
Demokrasia. Haki. Uhuru !!!
Napenda firigisi[emoji39][emoji39]
Kwahiyo imeshindikana kabisa kujibu maswali yangu pasi na kuniuliza swali?
Ipo mianaharakati uchwara ambayo haijui hata inapigania nini. Haitaki kushauriwa wala kusikiliza maoni ya wengine hata kama ni wengi. Imagine mijitu kama hii ndiyo ipate madaraka. Itashaurika na kusikiliza maoni ya wengine - hasa kama ni wengi? Je, huo siyo udikteta? Demokrasia ni nini kama siyo kusikiliza pia maoni ya wengine ili kuleta utangamano wa kijamii? Kama kila mmoja angefanya analotaka bila kujali uhuru wa wengine (hasa kama ni wengi) jamii ingekuwaje?Siasa zimeanza kukita kambi kwenye uzi huu na kuhatarisha kabisa uwepo wa huu uzi.
Tangu zamani tunajua kila mmoja ana itakadi yake, lakini tumeishi kwa kuheshimiana.
Ni kweli kuna wakati tunavikosoa vyama vya siasa lakini, tumedumu tukiheshimu ufuasi wa kila mmoja.
Ushauri wangu kwa wapenda siasa, Hoja zote za siasa zipelekwe kwenye majukwaa husika.
Wengine tumeamua kuwepo muda wote hapa maana kwenye jukwaa la siasa wengi wao hawana uwezo wa kujibu hoja za kisiasa, badala yake wamebakia kumwaga matusi na kukulazimisha kuwa ni wewe ni mfuasi wa chama furani hata kama sivyo hivyo.