Wakati nasoma taarifa ile, hisia zangu zikanirudisha kwenye kumbukumbu zangu za miaka 16 iliyopita katika Jiji la New York.
Kwa takriban miezi mitatu kati ya mwezi Februari na mwezi Aprili, mwaka 2004 mimi na Maalim Seif Sharif Hamad tulifanya ziara refu ya kikazi katika nchi takriban 13 ikiwemo Marekani, Canada na nchi za Ulaya Magharibi. Wakati huo Maalim Seif alikuwa Katibu Mkuu wa CUF na mimi nilikuwa ndiyo kwanza nimeteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Haki za Binadamu wa CUF ikiwa ni baada ya Mkutano Mkuu wa Chama uliofanyika mwezi Februari 2004.