Umefanya niwakumbuke warembo wawili mmoja wa kipare yule binti kaumbika jamani! Na kwao wote ni wazuri ile mbaya lakini yeye alikuwa kawazidi wote kwa uzuri, kwao walizaliwa wanawake watano wote. Yaani kuanzia sura hadi unyayo halafu alikuwa anajipenda sana. Ofisi zetu zilikuwa jirani yeye akiwa NBC na mimi nilikuwa na bank accounts zangu kwenye ile branch kumbe kila nikiingia pale branch ananicheck tu hadi siku nikamkuta nje akiwa kwenye break na nikamsalimia alivyokuwa anajibu basi mie sikufanya hiyana. Huyu nilimuita Halle Berry lakini Halle Berry wa ukweli haoni ndani, halafu kulikuwa na office mate wa Kichagga aliitwa Agnes huyu naye alikuwa bomba sana lakini alifariki baada ya ya kupata ajali akitokea Moro kurudi Dar kikazi RIP Agnes [emoji22][emoji22][emoji22]Mwenyezi Mungu anaumba jamani!!!