Huo utafiti kusema kweli hata mimi umenishangaza. Tafiti za wazungu hizi nyingine ni pasua kichwa [emoji16][emoji16][emoji16]
Nakumbuka kipindi fulani nikiwa mdogo sana kaka mkubwa ananilazimisha kuanza kwenda kula "hashikome" na wanaume huko nje eti nikiendelea kula na wanawake nitakuwa na tabia za kike. Kimbembe sasa huko nje kwa wanaume jamaa wako fasta balaa. Wewe mdogo kazi yako ni kutumwa tu. Na kabla hujaliweka sawa sawa bakuli la nyama jamaa wameshachangamka hasa kama ni wengi ambayo ilikuwa kawaida. Halafu ugali wa moto mno. Yaani we unahangaika kupoza jamaa wanatwanga tu. Mama akalitambua hilo akawa ananifichia nyama ananipa baadaye. Basi kuanzia hapo nikawa na nyodo kibao yaani...ila nilikuja kufumwa nimejibanza nafakamia nyama zangu za kufichiwa mama akapigwa mkwara hilo dili likafa [emoji51][emoji51][emoji51]
Kuwa mtoto wa mwisho kuna faida nyingi ila hasara kubwa ni kutumwa tumwa. Yaani hakuna kupumzika. Huyu anataka moto wa kuwashia sigara yake. Huyu maji. Huyu gogo akalie. Mwingine jembe lake aende shamba. Mara ndama sijui wameingia shamba la jirani. I hated it !!!