MFAHAMU DKT MPANGO _ Alizaliwa huko Buhigwe Kigoma mwaka 1957 mwezi July tarehe 14 Ni mchumi, amefanya kazi Benki ya Dunia, mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa iliyokuwa wizara ya Uchumi. Amelitumikia Taifa katika nyadhifa mbalimbali kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango kwenye serikali ya awamu ya 5. . Hivi sasa kinachosubiriwa ni Wabunge kupiga kura ili awe Makamu wa Rais. Spika Ndugai amesema utaratibu utakaotumika ni ule ambao ulitumika mwaka 2001 kufuatia kifo cha Dkt Omar Ali Juma ambapo Dkt Shein alipitishwa na Bunge kuwa Makamu wa Rais.