Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MPANGO AMSHUKURU MAMA SAMIA _ "Napenda kumshukuru sana Mh. Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kupendekeza jina langu na kuridhiwa na Chama chetu cha CCM ili liletwe hapa ili kuthibitishwa na bunge. Ni heshima kubwa sana, sikuwahi kuota."- Makamu wa Rais wa Tanzania Mteule, Dkt. Philip Mpango >>KutokaBungeniDodoma
 
MFAHAMU DKT MPANGO _ Alizaliwa huko Buhigwe Kigoma mwaka 1957 mwezi July tarehe 14 Ni mchumi, amefanya kazi Benki ya Dunia, mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa iliyokuwa wizara ya Uchumi. Amelitumikia Taifa katika nyadhifa mbalimbali kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango kwenye serikali ya awamu ya 5. . Hivi sasa kinachosubiriwa ni Wabunge kupiga kura ili awe Makamu wa Rais. Spika Ndugai amesema utaratibu utakaotumika ni ule ambao ulitumika mwaka 2001 kufuatia kifo cha Dkt Omar Ali Juma ambapo Dkt Shein alipitishwa na Bunge kuwa Makamu wa Rais.
 
AGUERO ANAONDOKA MAN CITY _ Man City wamethibitisha kwamba Mshambuliaji wao Raia wa Argentina Sergio Aguero (32) ataondoka Man City mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake kuisha akiwa ameichezea Timu hiyo kwa miaka 10.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…