Manchester City inafuatilia kwa karibu kuwasajili mshambuliaji wa Barcelona na Argentine Lionel Messi, 33, na mshambuliaji wa Borussia Dortmund, 20, raia wa Norway Erling Braut Haaland katika uwanja wa Etihad Stadium. (Sun)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba huenda akaondoka Manchester United hata pengine msimu huu huku Juventus ikiwa makini kumsajili mchezaji huyo na pia nia ya kumuuza mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27, katika makubaliano ya mabadilishano. (Tuttosport - in Italian)
Tottenham ina imani kubwa kwamba itaendelea kuwa na mshambuliaji wa England Harry Kane, 27, na wala haina mpango wa kumuuuza katika klabu nyingine ya Primia, huku Manchester City Manchester United zikiendelea kumnyatia. (Manchester Evening News)
Bayern Munich ina msaka mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min, 28, na iko tayari kumsubiri mchezaji huyo wa Korea Kusini ambaye sasa hivi yuko Spurs hadi msimu wa mwaka 2023 na pia amepewa ofa ya makubaliano ya muda mrefu na klabu ya London. (Football Insider)
Chelsea, Manchester United, Juventus na Real Madrid bado zinamtafuta mlinda lango wa Italia Gianluigi Donnarumma, 22, ambaye amekataa ofa mbili za mkataba mpya AC Milan. (Gianluca di Marzio, via Mail)
Barcelona inaonekana kuwa yenye uwezekano mkubwa wa kumsajili mlinzi Georginio Wijnaldum, 30, mkataba wake na Liverpool utakapomalizika msimu huu lakini klabu hiyo ya Catalan inakabiliana na ushindani kutoka Chelsea, Juventus na Paris St-Germain. Klabu hiyo ya Merseyside bado haijakata tamaa ya kuendelea kusalia kuwa wa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Uholanzi. (Marca)
Winga wa Crystal Palace Andros Townsend, 29, amesema kuwa klabu hiyo imemuarifu yeye pamoja na wachezaji wengine ambao hawana mkataba kwamba hatma zao hazitajadiliwa hadi mwisho wa msimu. (Talksport)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.