Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ripoti ya Utafiti ya Wageni wa Kimataifa ya mwaka 2016 (The 2016 International Visitor Exit Survey Report) iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Oktoba mwaka jana inaeleza kuwa upandaji wa milima ni kuvutio cha tatu kwa wageni wa nje wanaoingia nchini kwa mara ya kwanza baada ya utalii wa wanyamapori na ufukweni.
 
Uchambuzi zaidi za takwimu muhimu za mwaka 2016 za NBS (Tanzania in figures 2016) unabainisha kuwa milima tisa kati ya 10 mirefu zaidi nchini ipo katika mikoa miwili tu ya Kilimanjaro na Arusha. Ni mlima mmoja uitwao Mtorwi ndiyo unapatikana mkoani Iringa.
 
Ifuatayo ni orodha ya milima 10 mirefu zaidi Tanzania: -



Mlima Kilimanjaro, 5,895 (Kilimanjaro)

Mlima Kilimanjaro siyo tu ni mlima zaidi nchini bali katika bara zima la Afrika. Mlima huo wenye urefu wa mita 5,895 (futi 19,340) pia ni hifadhi ya Taifa. Hifadhi hiyo ina ukubwa wa kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini. Kilele cha Kibo ndio kivutio kikubwa kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na kufunikwa na theluji.

Mlima huo unaopatikana katika mkoa wa Kilimanjaro ni moja kati ya milima ambayo kilele chake hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka kila pande za dunia.
 
Mlima Meru, mita 4,566 (Arusha)

Mlima wa pili kwa ukubwa Tanzania ni Mlima Meru wenye kilomita za mraba 4,566 (futi 15064) kutoka usawa wa bahari ikiwa ni tofauti ya mita 1329 kutoka Mlima Kilimanjaro. Katika anga za kimataifa, Mlima Meru unashika nafasi ya tisa kwa urefu barani Afrika .
 
Mlima Meru unapatikana ndani ya Hifadhi ya Arusha ambayo ilianzishwa mwaka 1960. Baadhi ya wa wanyamapori waliopo katika hifadhi waliletwa kutoka katika maeneo mengine na hupenda kuzungukazunguka katika Mto Momella na Kreta ya Ngurudoto (Ngurudoto crater). Hifadhi hiyo ina ukubwa wa kilometa za mraba 137 na ipo umbali wa kilometa 35 kutoka mji wa kitalii wa Arusha na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
 
Back
Top Bottom