Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mlima Oldeani, mita 3,188 (Arusha/Manyara)

Mlima Oldeani unaopatikana katika mikoa miwili ya Manyara na Arusha una urefu wa mita 3,188 na kuufanya kuwa mlima wa sita kwa urefu nchini. Tofauti na milima maarufu ya Kilimanjaro na Meru, hakuna taarifa nyingi za kina kuhusu Mlima Oldeani.
 
Jaeger, mita 3,050 (Arusha)

Jaeger ni mlima wa nane katika orodha milima mirefu zaidi nchini. Mlima huu wenye urefu wa mita 3,050 unapatikana katika mkoa wa Arusha. Jaeger ni mlima wa nne kwa urefu mkoani humo baada ya milima Meru, Oldeani na Hanang. Tofauti na Mlima Meru, Jaeger hauna taarifa za kutosha za kuwasaidia watalii kujua kwa undani namna ya kutalii.
 
Monduli, mita 3,000 (Arusha)

Mlima Monduli una mita 3,000 upo katika mkoa wa Arusha ukiwa ni mlima wa tisa kwa urefu nchini. Huu ni mlima wa tano kwa urefu Arusha. Hii ina maana iwapo unataka kuvunja historia, unaweza kuipanda milima yote mkoani humo ukawa umeshapanda milima mitano kati ya 10 mirefu zaidi nchini.
 
Mtorwi, mita 2,961 (Njombe)

Watu wengi hudhani mlima Rungwe ni moja ya milima yenye vilele virefu zaidi hii ni kutokana na umaarufu wake lakini takwimu za NBS zinaonyesha tofauti. Rungwe unazidiwa urefu wa mita moja tu na Mlima Mtorwi kutoka mkoa Iringa ambao ndiyo mlima wa 10 kwa urefu Tanzania. Mtorwi wenye mita 2,961 ndiyo kilele cha Nyanda za Juu Kusini. Mlima Mtorwi ni sehemu ya platu ya Kitulo ambayo ni maarufu kutokana na maua yake.

Hata hivyo, mtandao wa lonelyplanet unasema miundombinu ya upandaji mlima hususan wakati wa masika siyo mzuri hivyo ni bora wapandaji wakafanya utalii wakati wa kiangazi
 
FB_IMG_1617462376951.jpg
 
Back
Top Bottom