Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maumivu ya nyonga wakati wa ujauzito ni jambo la kawaida wakati wa ujauzito. Huweza kutulizwa kwa kufanya mazoezi au kuwa na utaratibu wa kukaa au kusimama mgongo ukiwa umenyooka.
 
Wanawake wengi huwa wanaharibu mimba moja au zaidi katika maisha yao. Mara nyingi hawaelewi kuwa wameharibu mimba ila wanafikiri kuwa hedhi yao imechelewa na inaporudi huwa ya ajabu, ikitoa mabonge bonge ya damu. Ni wajibu wa kila mwanamke kuwa makini
 
Kichefuchefu au kutapika hutokea mara nyingi kwa wanawake wajawazito miezi mitatu ya mwanzo hasa nyakati za asubuhi. Kula vyakula vikavu kama mkate kabla ya kuamka kitandani. Pia usile ukashiba kula kidogo kidogo kila baada ya muda na epuka vyakula vya mafuta
 
Kalori ni kipimo kinachotumika kupima kiasi cha nguvu kinachotolewa na chakula. Mahitaji ya kalori kwa siku kwa wanaume ni kati ya kalori 2,000 na 3,000 & kwa wanawake ni kati ya kalori 1,600 na 2,400. Kuzidisha kalori husababisha kitambi (uzito kupita kiasi)
 
Ukiweza kunywa gilasi/bilauri ya maji badala ya chupa ya soda unaweza epuka kalori 150 zisizo za lazima na kukusaidia kupunguza uzito hadi kilo 7 kwa mwaka bila ya kufanya mazoezi
 
Kuangalia simu janja kwa muda mrefu hupunguza kiwango cha kukonyeza na kusababisha jicho kukaza kidigitali (digital eye strain) na kuacha macho yakiwasha, makavu na kuona mawenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…