Tafiti zimeonyesha kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama huwakinga watoto dhidi ya kuwa na uzito uliozidi na unene uliokithiri wanapokuwa wadogo na hapo baadae
Maradhi ya Michezo ya Video & Simu (Gaming Disorders) yanatarajiwa kuwekwa kwenye orodha ya WHO ya maradhi ya akili. Mtu anakuwa na maradhi hayo ikiwa hucheza michezo hiyo kwa muda mrefu na kuathiri maendeleo yake ya kitaaluma au kuathiri utendaji kwa wafanyakazi.
Mwanamke huzalisha mayai yenye aina moja ya kromosomu inayotambulika "XX" na hayo huendeleza jinsia ya kike. Kromosomu yoyote ya mwanamke ikirutubishwa & kromosomu "X" ya mwanaume hutengeneza "XX" ambayo ni mimba ya mtoto wa kike
Kromosomu (chromosome) ni nyuzinyuzi katika kiiniseli cha kila kiumbe ambazo hubeba viiniurithi yaani jeni (gene). Kromosomu yoyote ya mwanamke ikirutubishwa & kromosomu Y ya mwanaume hutengeneza "XY" ambayo ni mimba ya mtoto wa kiume
Licha ya maendeleo makubwa ya teknolojia bado baadhi ya taasisi na mashirika ya umma yanatoa taarifa kwa umma kwa njia za kizamani kitu kinachofanya watu wengi kukosa haki ya taarifa muhimu
Sio tu kwamba chakula bora husaidia kukinga maradhi, bali pia husaidia mwili kupigana na maradhi na kumfanya mtu apone haraka. Kwa hiyo chakula bora ni kitu muhimu wakati mtu anapokuwa mgonjwa
Taasisi zetu za umma zinahitaji kwenda na wakati & mabadiliko ya teknolojia kwenye kufikisha taarifa muhimu kwa umma ili kuwafikia wengi. Ufahamu ni nguvu ya maamuzi chanya
Vitamini D ambayo mara nyingi hutokana na mwanga wa jua ni muhimu kwa kuimarisha mifupa na ubongo. Ila tafiti za hivikaribuni zimedai vitamini hiyo huimarisha kinga ya mwili na kumkinga mtu dhidi ya maradhi ya mfumo wa upumuaji kama mafua.
Kutumia muda pamoja na watu unaowapenda hukufanya uwe na furaha hata kucheka sana. Wataalamu wanadai kicheko ni tiba bora kwa afya inayodhoofu kwa maana huchochea kinga ya mwili, hushusha shinikizo la damu na kuamsha utendaji mzuri wa ubongo.
Wengi hufikiri kwamba anayewakaba wakiwa usingizini ni jini lakini tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama “mwili kupooza usingizini”. Tendo hilo huwa linakutokea katika muda wa sekunde 20 lakini wewe unayehusika utahisi kama dakika 5 au 10
Kulingana na utafiti upweke ndio chanzo kikuu cha kupungua thamani/ubora wa maisha ya wazee, kutia ndani huzuni, akili kudhoofu (kupoteza kumbukumbu) na maradhi ya mishipa & moyo yanayoweza sababisha kifo cha ghafla.
Wenzi kulala pamoja huleta faida nyingi kama kuimarisha mahusiano, kutatua matatizo na kuweka mikakati ya mafanikio. Kukumbatiana huongeza utolewaji wa homoni za upendo & furaha hivyo kuwafanya wenzi kuwa na usingizi mnono
Watafiti wamebaini kuwa na malengo maishani husaidia mtu kuishi umri mrefu kwa maana kuwa na malengo hupunguza hatari ya kuugua, usingizi mnono na kuwa na tabia zinazochochea afya bora