Wenzi wanaotembea, kimbia au kufanya mazoezi pamoja hawapati tu faida za kiafya kwa kuushughulisha mwili bali wanajenga ukaribu zaidi hivyo kuboresha mahusiano yao, kulingana na watafiti
Kufanya mazoezi huimarisha mwili na ogani zake kama moyo. Mazoezi humuepusha kuwa na uzito kupita kiasi, huzuia maradhi ya moyo na kupanda kwa shinikizo la damu na kuboresha kumbukumbu na utendaji mzuri wa ubongo/akili
Kuamka alfajiri na kujiandaa ipasavyo kwa ajili ya siku yenye mafanikio husaidia kuwa na amani ya akili na moyo kuliko kuamka umechelewa ambapo utafanya kila kitu kwa pupa hivyo kusababisha mkazo (stress)
Dimples (vibonyo vidogo) hupendeza sana usoni mwa mtu ila huwa ni matokeo ya kurithi kasoro ya kijeni (genetic flaw) ambapo tishu zinazounganisha ngozi na nyama kwenye mfupa wa taya zinabonyea
Kutembea na kuendesha baiskeli hukupa fursa ya kufanya mazoezi bila kuhitaji muda maalumu wa kufanya mazoezi. Kuendesha baiskeli kwa saa 1 kila siku kwa siku 7, hukusaidia kuchoma nusu kilo ya mafuta kutoka katika mwili wako
Kufanya kazi sana au kusoma sana huku unaumwa kunaweza kupunguza ufanisi na kuharibu ubongo. Unapojihisi kuumwa ni vyema kupata tiba kwanza ndipo uendelee na kazi zako
Wanasema sigara ni hatari kwa afya ila kwanini wengine wanavuta sigara toka vijana hadi wanazeeka? Watafiti waligundua wavutaji wanaoishi hadi umri mkubwa wana chembe za urithi (jeni) maalum zinazo chochea maisha marefu ila bado uvutaji sigara ni hatari kwa afya yako.
Nyanya zina kiwango kikubwa cha Vitamini C na virutubisho vingine ambavyo hufanya kazi ya kusafisha mwili na kutoa sumu pia. Kutokana na virutubisho hivyo nyanya husaidia kuharibu viini (free radicals) ambavyo hupelekea kutokea kwa saratani.
Mambo matano rahisi yanayoweza kukufanya uwe na furaha: 1~ Kutafakari (Meditation), 2~ Kutabasamu, 3~ Kufanya Mazoezi, 4~ Kusaidia Wengine & 5~ Kuwa na Malengo!
Watafiti wamedai wanafamilia wanaokula pamoja wanapata faida nyingi za kiafya kutia ndani kuboresha uwezo wao kiakili, kuwa na uzito unaofaa kiafya, kupunguza hatari ya kupatwa na sonona (depression), kupunguza hatari ya kutumia dawa za kulevya n.k!