Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20, ni mchezaji anayelengwa zaidi na Barcelona kwa sasa.Timu hiyo ya ligi ya Uhispania ingependa kusaini mkataba nae katika msimu wa kiangazi lakini itasubiri mwaka ujao kama kutakuwa na haja ya kufanya. (Mundo Deportivo - in Spanish)
 
Juventus inataka kusaini upya mkataba na mshambuliaji wa Everton na Italia Moise Kean, ambaye yuko katika mkataba na Paris St-Germain. The Toffees wanataka euro milioni 50 (£43.5m) kwa ajili ya Kean, 21, au mkataba wa kubadilishana wachezaji unaomuhusisha kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 26, au kiungo wa kati-nyuma wa Uturiki Merih Demiral, 23. (Gazzetta - in Italian)
 
Sporting Lisbon wanataka kumchukua mchezaji wa safu ya nyuma-kulia wa Uhispania Pedro Porro kwa mkataba wa kudumu ambaye yuko Manchester City na kufanya mkataba wa makubaliano ya kumnunua kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 wa euro milioni 8.5 (£7.4m).(Goal)
 
Newcastle wanahofia hali ya mkataba wa Jacob Murphy licha ya kuwa na nia na winga huyo wa English kutoka kwa klabu za Watford na Rangers. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 unaisha mwaka 2022. (Chronicle)
 
Arsenal huenda wakampatia mkataba kiungo wa kati-nyuma David Luiz, 33, huku meneja Mikel Arteta akiwa makini kumpa fursa zaidi mlinzi wa Mfaransa William Saliba, 20, katika mechi za kabla ya msimu baada ya mkataba wake katika klabu ya Nice kumalizika. (Football.London)
 
[emoji16][emoji16] Utopolo bana...
IMG-20210415-WA0025.jpg
 
Back
Top Bottom