"Hotuba imeisha. Tumeisikia. Penye wengi kuna mengi. Nimetoka na haya: 1. Hotuba nzuri lakini ya kawaida. Wakuu wa nchi wa kawaida huongea kwa uungwana mbele ya mabunge. Yaliyo mengi tumeyashika tangu utoto. Yalienda likizo awamu ya tano" Askofu Dkt. Benson Bagonza,
"Mwisho wa mwezi, Mama anakalia kiti cha chama dola chetu. Baada ya hapo akutane na vyama vya siasa. Akiwa nao atasahau kuwa yeye ni Mwenyekiti wa chama dola? Mashaka ni makubwa kuliko matumaini" Askofu Dkt. Benson Bagonza, Askofu Mkuu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Karagwe
"Kuna vitu nimevikosa na ni haki nivikose kwa sababu hotuba sikuandaa mimi. Nilitamani: -Katiba mpya aliyoiongoza -Maridhiano na wahanga wa awamu Iliyopita -Matamko yaliyokiuka katiba na yanaendelea kutekelezwa -Uhuru wa vyombo vya habari" Askofu Dkt. Benson Bagonza
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.