Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ana kashfa gani huyu dogo maana naona makamanda wamefurahi kweli kweli...
Dogo huyu, kuna nyuzi nyingi kwenye jukwaa la siasa zilifunguliwa tangu zama za marehemu, zikimuhusisha na uporaji kwenye maduka huko Hai na na jijini Arusha.
Pia alihusika kuteka watu, kupiga na kujeruhi.
Kuna picha ya jamaa mmoja iliwekwa amekatwa masikio na huyo DC.
Kuna madai pia alikuwa muonevu lakini hakuwa akimtii mkuu wake wa mkoa mama Anna Mgwira.
Inadaiwa alikuwa untouchable, kwakuwa alipewa kila aina ya ulinzi na aliyemteua, ambaye kwa bahati mbaya sana hivi sasa hayupo tena.
Kwakweli watu huko siasani wanafurahia Iddi sambamba na kung'olewa bwamdogo huyo.
 
Pole imfikie hakujua kwamba Cheo ni dhamana.
 
Pole imfikie hakujua kwamba Cheo ni dhamana.
Wengine wanapewa mavyeo haya wakiwa bado wadogo mno tena bila mafunzo na exposure yo yote. Nimesoma mahali watu waliosoma naye huko Ikizu sekondari Musoma wanasema alikuwa mbabe hivi hivi na hakujificha kuwa ni mtu wa usalama wa taifa tangu zamani.

Ni muda wa kukua na kujifunza kuhusu maana hasa ya maisha, madaraka na muda...
 
Makonda kwenye kumbukumbu yake ya kuzaliwa Steve Nyerere ndiye aliyemkumbuka bongo movie wengine wamempotezea kweli wakati si lele
Naamini huyu naye akipewa madaraka tena atakuwa tofauti na ujinga na majigambo yale ya kitoto yatakuwa yamemwisha. Ametoka mbali sana na mama na anaweza kupewa ukuu wa mkoa tena. Sema tatizo mama inavyoonekana anaogopa sana kusemwa mitandaoni na anajaribu kupendwa na kila mtu. Akimpa madaraka tena huyu najua mitandaoni humu kutawaka moto na mama sidhani kama anataka hilo. Ngoja tuone!
 
Kwakuwa vyeo hivi ni utumishi wa uma, na uma umeonyesha kuwakataa kutokana na vitendo vyao, kwakweli hakuna namna, mama aachane nao tu.
Mbona Jokate Mwegelo anasifiwa, mbona Mtaka anasifiwa, mbona Martin Shigella anakubalika!! hawa wengine waachwe wafanye biashara zao serikalini kumewashinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…