Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"


Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu, amesema kuwa ni muhimu Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita ukawa na magari maalum ya kubeba abiria.MBUNGE WA GEITA MJINI, CONSTANTINE KANYASU.
Amesema mtu anasafiri na ndege anashuka uwanja wa Ndege Chato alafu anatakiwa kusafiri umbali wa Kilomita 110 hadi Geita mjini na Kilomita zaidi ya 10 hadi Chato mjini.
"Ili abiria waendelee kuwepo kwenye ndege zetu lazima Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) likawa na 'shuttle' za kubeba abiria,"amesema.
 

Mbunge ataka uchunguzi mtambo wa kutengeneza barakoa
MBUNGE wa Viti Maalum, Agnesta Kaiza ameiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina wa mtambo wa kutengeneza barakoa ulionunuliwa na Bohari ya Madawa nchini (MSD), kutokana na kutofanya kazi kwa ufanisi.
1621408639244.jpeg

MBUNGE WA VITI MAALUM, AGNESTA KAIZA.
Akichangia bungeni leo hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka 2021/22, Kaiza amesema mtambo huo ulinunuliwa kwa dharura na kuigharimu serikali zaidi ya Sh.milioni 600 lakini unazalisha kwa kiwango cha chini.
Amesema mtambo huo ulitakiwa kuzalisha barakoa milioni nne kwa mwezi lakini hadi Septemba mwaka jana ulizalisha barakoa 320,000.
“Mpaka sasa mtambo huu umezalisha asilimia nne ya uwezo wake.Naiomba Serikali ifanye uchunguzi wa kina kuhusiana na ununuzi wa huo mtambo wa kutengeneza barakoa wa MSD,tumenunua kwa pesa nyingi lakini cha kushangaza mtambo huo umekuwa ukizalisha chini ya kiwango," amesema.
 
Mwanafunzi adaiwa kujitoa ujauzito kwa kijiti
MWANAFUNZI anayesoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Uzogole Manispaa ya Shinyanga (jina limehifadhiwa), amedaiwa kujitoa ujauzito kwa kijichokonoa na kijiti, ili aendelee na masomo.
Imeelezwa mwanafunzi huyo alipata ujauzito huo wakati akiwa nyumbani akisubiri matokeo ya kidato cha kwanza, na alipofaulu akaingia nao sekondari, ndipo Januari mwaka huu akaona autoe ili asifukuzwe shule.
 
Askari Polisi Kata wa Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga ilipo shule hiyo, Emmanuel Maganjila, ilibainisha hayo juzi kwenye kikao cha kujadiliana kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye kata hiyo, kilichoandaliwa na Shirika la YWCA.
Alisema mwanafunzi huyo alifanikiwa kujitoa ujauzito huo, na kwamba kilitoka kiumbe kikiwa kimekufa, lakini mwanafunzi huyo aliwahishwa hospitali kwa ajili ya matibabu, na sasa anaendelea na masomo
 
"Natoa wito kwa wazazi mkoani Shinyanga vunjeni ukimya, zungumzeni na watoto wenu na kuwapatia elimu ya makuzi na madhara ya kufanya ngono katika umri mdogo," alisema Maganjila.
Naye Katibu wa Shirika la YWCA, Marysiana Makundi, ambao wanatekeleza mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye Kata ya Ibadakuli, alisema matatizo hayo ya mimba za utotoni ili kuisha, inapaswa wahusika wawe wanafungwa jela badala ya kuachiwa huru.
 
Alisema mbali na utoaji wa elimu ya kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia, wazazi wamekuwa kikwazo, kutokana na kuwa na tabia ya kumaliza kesi kimya kimya na watuhumiwa ambao huwapatia ujauzito wanafunzi, kwa kupeana fedha ama mifugo na kusababisha kesi kufutwa mahakamani kutokana na kukosekana ushahidi.
 
Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Ibadakuli, Mwijage Patrick, aliwataka wazazi mkoani Shinyanga, waachane na mila kandamizi, ambazo zimekuwa zikimnyima haki mtoto wa kike, kwa kuonekana hastahili masomo bali ni wa kuolewa tu, na ndio chanzo cha mimba na ndoa za utotoni kuendelea kwa kasi mkoani humo.
 
Back
Top Bottom