Huu hutokana na vyakuwa vya mafuta tunabyokula na kutofanya mazoezi kuondoa mafuta hayo, kutopata choo ipasavyo na ulaji wa chunvi nyingi na vitu vya sukari nyingi kama ice cream, chokleti nk.
Wekeza Kwenye Afya yako sasa na hata kama ishaathirika na magonjwa hayo ipo njia ya kuweza kukusaidia kurudisha afya kutegemea na kiasi gani umeathirika , hivyo usikate tamaa tafuta afya yako nayo utaipata.
Kujua namna ya kutunza afya yako hasa kwa wakati huu ambao kupata vyakula na namna ya kuboresha afya ni changamoto kutokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha
Hakuna kitu kina kera kama matizo yanayo sumbua watu duniani kwa wakati huu kama maswala ya kutetereka kwa afya na kuandamwa na magonjwa mengi ambayo yanakatisha na kufupisha maisha ya watu wengi na kuifanya dunia kuwa kwenye taharuki na mahangaiko ya namna gani watakabiliana na matatizo hayo ya kiafya.
Takwimu za shirika la afya duniani (WHO) zinaonyesha utafiti wake wa mwaka 2000 hadi 2019 kuwa dunia nzima vifo 7 kati ya 10 vilisababishwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Hivi vifo saba vinahesabika kwa 44% ya vifo vyote duniani au 80% ya vifo vya kila watu 10 na kwa magonjwa yote yasiyo ya kuambukiza yanahesabika kuwa 74% kwa vifo vyote duniani.
Hivyo wana sayansi na wachunguzi mbalimbali wanajaribu kuchunguza tatizo ni nini na watu wafanyeje kujitoa katika matatizo ya kiafya au kutoingia huko kabisa na wale waliotoka huko wasirudi kabisa.
Hapo ndipo ilipo gundua kuwa mitindo wa maisha ndio chanzo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza na mabadilko yake ndio yanaweza kusaidia watu kutoka kwenye matatizo hayo au kutoingia kwenye matatizo hayo kabisa.