Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2021-05-22 epl standings - Google Search.png
 
huyo kiranga ana balaa, kwanza anapenda ligi.
malcom anapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kila kijana, ubongo wake umejaa info
nyani, ingilishi yake ni ya kuishi zaidi, sidhani kama ana upeo mkubwa unaotokanwa na kusoma sana.
sidhani kama anakuzidi wewe kiupeo wa kufikiri na kujenga hoja
Ndugu yangu. Labda umezidisha urojo leo. Mimi hata robo siifikii hiyo miamba ya ngeli, falsafa, hoja na mantiki. Hata kwenye maisha halisi ni hivyo hivyo. Raha yangu jioni kwenye magenge ya tangawizi kule Mbagala tukifungana kamba za kila aina na kuilaumu serikali. Maisha ni marahisi sana ukiyajulia (na hapa siongelei pesa)

Wewe mwenyewe hapo ni moto wa kuotea mbali. Unajua mambo mengi mno mpaka huwa nakuogopa ukisema eti ndo kwanza bado uko chuo (labda chuo cha TISS). Ukija kufika huku kwenye 70+ huku sijui itakuwaje.

Mungu Amegawa karama zake kwa kila mmoja wetu kwa kiwango chake na kwa namna ya pekee sana. Tukilitambua hili tutaheshimiana huku tukijua kuwa karama zetu hazina thamani sana katika upekee wake bali zinang'ara kama kurunzi angavu katika usiku wenye giza totoro pale tu zinapochanganywa pamoja. Na hii imekuwa ndiyo nguzo kuu na falsafa-mama ya uzi huu mpaka tumejenga urafiki na undugu humu. Mungu Aendelee kutubariki [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Tutafanya usajili, sina hofu na hilo. Ingawa Kane sitaki aje UNITED!
Wtu wanaongea ana kuhusu Kane kuja UNITED
tutahitaji takribani paundi millioni 300 za usajili ili kukamilisha maeneo yote muhimu endapo kane ataidhinishwa kwenye usajili
  1. anahitajika sancho
  2. anahitajika mlinzi wa kati
  3. anahitajika kiungo mkabaji
  4. umuongeze na kane. sidhani kama litawezekana usawa huu wa corona,
 
Ndugu yangu. Labda umezidisha urojo leo. Mimi hata robo siifikii hiyo miamba ya ngeli, falsafa, hoja na mantiki. Hata kwenye maisha halisi ni hivyo hivyo. Raha yangu jioni kwenye magenge ya tangawizi kule Mbagala tukifungana kamba za kila aina na kuilaumu serikali. Maisha ni marahisi sana ukiyajulia (na hapa siongelei pesa)
umeamua kujilinda vya kutosha, baadae ukanisukumia paka wa uso.
acha nikubaliane na maneno ya aliyenizidi, mara nyingi hujawa na hekima pamoja na uongofu
 
Kaangalie comment ya #27. Nimecheka hatari [emoji1727][emoji1727][emoji1727][emoji1734][emoji1734][emoji1734]

Lakini seriously, hili lina ukweli wo wote?
 
Back
Top Bottom