Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unachoona kigumu kwao wanahisi si ugumu bali ni changamoto za kuzidisha jitihada na umakini tu. Kwenye mapenzi pia hali haiko tofauti sana. Wale wanao achana kila siku si kama ndiyo wanakosewa sana kuliko wale ambao hawaachani, hapana. Suala ni lile lile tu.
 
Wakati wengine wakiona tofauti zao ni kama changamoto za kusomana tabia na kuamua kuishi kutokana na kila mmoja kumjua mwenzake. Wenzao wanaona suluhisho la yote ni kila mmoja kuwa na maisha yake. Suala la uvumilivu kwao hamna.
 
Hakuna mapenzi duniani yanayoweza kushamiri bila suala hili. Usipokuwa na moyo wa uvumilivu katika mapenzi basi kila mtu utamuona hafai. Utamuona hafai na kila siku utakuwa mtu wa kuanzisha mahusiano mapya. Hayo si maisha sasa!
 
Mahusiano yaliyodumu si kwa kuwa wahusika hawakoseani au makosa wanayokoseana ni madogo sana. Hapana. Kila binaadamu ana mapungufu yake. Wote huwa wanakoseana ila tofauti yake na wengine ni kwamba busara na uvumilivu huwa msingi wa mapenzi yao na ndiyo maana tunaona wanadumu mpaka leo.
 
Hivyo unavyotaka kuachana na uliye naye suala la kujiuliza ni kuwa mara ngapi umemueleza kuhusiana na suala unalotaka kumuachia. Na hiyo isitoshte tu pia jiulize ni sababu gani inayomfanya kutenda suala hilo. Ukimaliza hapo rudi nyuma na jiulize tena huwa unatumia maneno ya aina gani katika kumkanya.
 
Maana wengine baada ya kukosewa wao huwa hawawakanyi vyema wenzao wao bali huripuka kwa maneno makali na dharau. Matokeo yake sasa wahusika badala ya kuwasikiliza na kufanyia kazi maneno wanayoambiwa kutokana na makosa yao. wao huwapuuzia na kwaona ni wasema hovyo.
 
Ndiyo, kukosewa kunaumiza sana ila jiulize ni kitu gani kimetokea bila sababu? Kwenye makosa ya mpenzi wako kuna sababu nyuma yake, hebu itafute badala ya kulalamika.
 
Kwa kuwa huyo uliye naye unampenda kwa dhati basi amua kwenda naye taratibu ukijitahidi kumbadilisha tabia zake. Usiogope, inawezekana, suala ni uvumilivu na kujiamini tu. Kukubali kumpoteza unayempenda kwa kukosa uvumilivu ni kujitakia kuingia katika maisha ya kutanga tanga tu.
 
FB_IMG_1621374295072.jpg
 
Back
Top Bottom