Kipindi nasoma, naishi home kwa wazee, mfanyakazi wa ndani aligundulika ana mimba. Ikabidi ahojiwe muhusika ni nani. Ile nyumba watoto wa kiume tulikuwa watano ( kuna mtoto wa baba mdogo nae alikuja kutembea maana alikuwa likizo chuo). Kulingana na mazingira ya pale home, sio rahisi yule dada...
Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.
UKOSEFU WA CHOO.
Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumboni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo.
Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.
UGONJWA WA MOYO.
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!
SHINIKIZO LA DAMU.
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.
UGONJWA WA MAPAFU.
Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.