Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1622831362972.jpg
.
 
😀😀 basi jamaa mara ya mwisho namuona clouds alikuwa kipande cha mtu na kitambi kilikuwepo
kumbe basi sikuwa namfatilia hata jojo ila juzi kati hapa zimezuka sifa nyiingi kwake nikaenda muangalia kabadili nini sijaona kipya sijui ndo kumtafutia uteuzi zaidi au kumlinda. makonda ndo kabisaa tangu bongo movies waache shobo kwake sizion picha zake😂😂😂😂
 
MSIMU wa Ligi Kuu England wa 2020-21 umeshafika tamati kwa Manchester City kunyakuwa ubingwa. Na sasa kila klabu inajiandaa na msimu ujao kwa kupiga hesabu za kunasa mastaa wa maana watakaokuja kuleta ushindani kwenye ligi hiyo.
 
Harry Kane

Ni suala la lini atahama, hiyo ndio ishu inayomkabili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane. Fowadi huyo wa kimataifa wa England aliripotiwa kuwaambia mabosi wa klabu yake ya Spurs kwamba anataka kuondoka kwenda kujiunga na timu itakayompa nafasi ya kubeba mataji na jambo hilo limezifanya klabu za Manchester City, Manchester United kuwania huduma yake. Ukiziweka kando timu za England, Real Madrid, Juventus, Bayern Munich na Paris Saint-Germain ni timu nyingine ambazo zimetajwa kuwania saini ya mchezaji huku, Man City ikipewa nafasi kubwa ya kunasa huduma yake. Bosi wa Spurs, Daniel Levy, alisema anamuuza Kane kwa Pauni 200 milioni.
 
Erling Haaland

Man City na Man United zimekuwa zikihusishwa na mpango wa kumsajili straika wa Borussia Dortmund, Erling Haaland, hasa baada ya kuonyesha makali kwa msimu huu, ambapo alifunga mabao 41. Haaland anaweza kupatikana kwa ada ya Pauni 68 milioni tu mwakani kutokana na kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wake. Lakini, ushindani wa kupata huduma yake kwa mwakani utakuwa mkubwa sana, hivyo timu zote zinapambana vikali kunasa saini yake kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi, licha ya kwamba huenda akaigharimu timu itakayonasa saini yake mkwanja wa Pauni 100 milioni.
 
Kylian Mbappe

Huu ni usajili ambao mashabiki wa Liverpool wanausubiri kwa hamu kubwa kuona unatokea kwenye klabu yao katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Supastaa wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe bado hajasaini mkataba mpya na huu wa sasa utafika tamati mwakani, hivyo hakuna namna zaidi ya kumuuza tu kama hatakuwa amesaini dili jipya. Staa Mbappe amekuwa kwenye rada ya timu kadhaa ikiwamo Real Madrid, ambao ndiyo wanaotajwa kuchuana vikali na Liverpool kwenye mchakamchaka wa kuwinda huduma ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. Licha ya Mbappe kubakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, huduma yake haiwezi kupatikana kirahisi, lazima itavuka Pauni 100 milioni.
 
Mohamed Salah

Liverpool haikuwa na wakati mzuri sana kwenye Ligi Kuu England msimu huu, lakini mambo hayakuwa mabaya kwa mshambuliaji wao, Mohamed Salah. Salah alionyesha kiwango bora kabisa ndani ya uwanja na kuchuana kwenye vita ya kuwania Kiatu cha Dhahabu, ambapo alizidiwa bao moja tu na Harry Kane. Mkataba wa supastaa huyo wa Misri utafika tamati 2023 huko Anfield, lakini mambo yanaweza kugeuka na akapigwa bei kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi kama kutakuwa na ofa ya maana itakayowekwa mezani huku klabu kama Juventus, Real Madrid, Paris Saint-Germain na Bayern Munich zikihusishwa na saini yake.
 
Paul Pogba

Man United imekuwa na msimu mzuri kwenye Ligi Kuu England na kumaliza kwenye nafasi ya pili, huku wakifika fainali ya Europa League ambapo walichapwa kwa penalti 11-10 na Villerreal baada ya sare ya bao 1-1 katika muda wa dakika 120. Kwenye mafanikio hayo, kiungo Paul Pogba alihusika kwa namna moja au nyingine.
 
Lakini, shida inakuja sehemu moja tu, Man United haina uhakika kama itafanikiwa kubakiza huduma ya kiungo huyo kwenye kikosi chao kutokana na kubakiza miezi 12 tu kwenye mkataba wake. Kama Pogba atashindwa kusaini dili jipya kwenye majira haya ya kiangazi, Man United haitakuwa na namna nyingine zaidi ya kumuuza wakati dirisha litakapofunguliwa ili kukwepa hasara ya kumpoteza bure kabisa mwakani.
 
Jadon Sancho

Man United inaweza kumpoteza kiungo wake Paul Pogba, lakini miamba hiyo ya Old Trafford inatarajia kujiimarisha kwenye safu yake ya ushambuliaji kwa kumleta Jadon Sancho kundini. Man United ilifanya kila inachoweza kujaribu kunasa huduma yake kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka jana, lakini ada ya Pauni 108 milioni iliwafanya Man United kuishia njiani kwenye kukamilisha dili hilo.
 
Kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi atapatikana kwa gharama ya chini, hivyo Man United inapata uhakika mkubwa wa kunyakua saini yake akacheze upande wa kulia ili kuwapa nguvu kwenye harakati zao za kufukuzia taji la Ligi Kuu England msimu ujao.
 
Back
Top Bottom