Harry Kane
Ni suala la lini atahama, hiyo ndio ishu inayomkabili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane. Fowadi huyo wa kimataifa wa England aliripotiwa kuwaambia mabosi wa klabu yake ya Spurs kwamba anataka kuondoka kwenda kujiunga na timu itakayompa nafasi ya kubeba mataji na jambo hilo limezifanya klabu za Manchester City, Manchester United kuwania huduma yake. Ukiziweka kando timu za England, Real Madrid, Juventus, Bayern Munich na Paris Saint-Germain ni timu nyingine ambazo zimetajwa kuwania saini ya mchezaji huku, Man City ikipewa nafasi kubwa ya kunasa huduma yake. Bosi wa Spurs, Daniel Levy, alisema anamuuza Kane kwa Pauni 200 milioni.