D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,665
- 121,102
La msingi katika mazungumzo ya Daruweshi ni kule kuelezea kwake bila ya kuweka ushahidi au vielelezo vyovyote vile kuwa: “Labda ni vyema ikajulikana tangu mwanzo kwamba kamati iliyoundwa na Karume ya kuongoza mapinduzi hayo, ilikuwa na jumla ya watu 14.”
Walipotembeleya Cuba katika mwezi wa Mei 1964, Shirika la Habari la Cuba liliwafanyiya mahojiano memba wawili wa Kamati ya watu 14, Ramadhani Haji na Saidi Idi Bavuai yenye kutowa mwangaza mzuri juu ya maandalizi ya Mapinduzi ya Zanzibar. Baada ya kutowa historia fupi ya Afro-Shirazi kutokeya mwaka 1957 walielezeya matukio yaliofikiya kupinduliwa kwa Sultan Sayyid Jamshid bin Abdullah:
Uchaguzi ulipofanyika mwaka 1963 chini ya utawala wa kikoloni wa Kiingereza, chama cha Afro-Shirazi kilishindwa na kiliunda kamati ya kufanya mapinduzi. Baada ya uchaguzi kikundi kidogo cha chama cha Afro-Shirazi kiliungana na Chama cha Kizalendo (Nationalist Party). Haya mapinduzi ya watu 14 hayakuungana wakati wowote ule na chama chochote chengine kikiwemo chama cha Afro-Shirazi…hata chama cha AfroShirazi chenyewe kilikuwa hakielewi kinachoendelea